Home »
» Waziri Simbachawene; tuenzi mambo mema yalioachwa na Mrema
Waziri Simbachawene; tuenzi mambo mema yalioachwa na Mrema
Na Mwandishi Wetu Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameomba wananchi kuenzi mambo mema yaliyoachwa kama alama wakati wa uhai wa Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
“Tunamkumbuka kwa uzalendo wake wa kupenda demokrasia, lakini pia kupenda amani na utulivu katika itikadi zote. Mrema ni mtu mwenye rekodi kubwa katika siasa za ushindani wa nchi yetu”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya hayati Augustino Lyatonga Mrema iliyofanyika Marangu – Vunjo Mkoani Kilimanjaro.
"Sisi kama serikali tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu; kushiriki msiba kwa moyo mkuu maana sisi sote tunakwenda safari hiyo, yeye ametangulia sisi tupo nyuma yake, alisema waziri."
Ameeleza serikali na viongozi wakuu wanawapa pole Mama Watoto wa Marehemu na Wanakiraracha kwa ujumla na kipekee sana wanachama wote wa TLP, chama ambacho amefariki akiwa ni Mwenyekiti wake wa Kitaifa.
“ Marehemu Mrema amefariki akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole,na amefanya kazi yake vizuri alisema Waziri”
Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mhasham Baba Askofu Ludovick Minde, Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Padre Deogratius Matiika wakili wa Askofu Jimbo Katoliki Moshi ametoa pole kwa wanafamilia na wale wote walioguswa na msiba.
Sisi kazi yetu kubwa ni kuendelea kumuombea ili Mwenyezi Mungu ampe furaha mbinguni, ameshiriki na sisi katika maendeleo ya jimbo letu, na tunashukuru Mungu kwa hayo aliyoyafanya.
“Nawaomba wanafamilia Mshikamane baba ameondoka msije mkagombana, mkae kwa amani na upendo, alisema Padre Matiika”
Related Posts:
CHAMWINO YAJIWEKEA MPANGO MKAKATI WA KUONDOA ZIRO MASHULENINa Peter Mkwavila CHAMWINO. MKUU wa wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Gift Msuya amesema kuwa ili kuepukana na ziro shule za masingi na sekondari wamejiwekea mpango mkakati wa kuwasaka watoto wasioenda shule na ikiwemo na k… Read More
SHAKA ATAKA WATUMISHI SIKONGE KUFIKA KWA WANANCHI KUSIKILIZA CHANGAMOTONa Mwandishi Wetu, Sikonge KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wilayani Sikonge kwenda kutatua changamoto walizonazo… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 19, 2022… Read More
WATENDAJI WA SENSA WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDIINa mwandishi wetu Watendaji wa Sensa wapewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 August 2022, wito huo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi … Read More
JIFUNZE KUHUSU MTI UNAFUNDISHA MENGI Na.Mwl Triple J. "Basi *KWA MTINI JIFUNZENI* mfano; *TAWI LAKE likiisha KUCHIPUKA NA KUCHANUA MAJANI* , mwatambua ya kuwa *WAKATI WA MAVUNO U KARIBU"*(Mathayo 24:32) ...MAISHA Ya MWANADAMU ni Kama MTI, Matendo Yake … Read More
0 Comments:
Post a Comment