Kiwanda
cha kuchenjua Madini ya Shaba kinatarajiwa kuanzishwa wilayani Tunduru
Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha shughuli za kuchenjua madini hayo
kufanyika nchini na hivyo kulinufaisha taifa na watanzania.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko leo Agosti 16, 2022
mkoani Mwanza alipokutana na Kampuni ya Mineral Access System Tanzania
Limited inayotarajia kujenga kiwanda cha kuchenjua madini ya Shaba
katika eneo la Mbesa wilayani Tunduru.
Dkt.
Biteko, amewapongeza kuwekeza nchini kwani uwepo wake utasaidia
kuongeza thamani ya madini na hivyo kuongeza tija ya kiuchumi kwa taifa
na kwa wanachi wa Tunduru.
Amesema,
Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji ili kuwekeza katika Sekta ya
Madini kwa kuwa tayari imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwenye
mnyororo wote wa shughuli za madini ikiwemo shughuli za utafiti,
uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini bila changamoto yoyote.
"Serikali
kupitia Wizara ya Madini itaendelea kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza
katika Sekta ya Madini ili Watanzania wanufaike na rasilimali hiyo,"
amesema Dkt. Biteko.
Vile
vile, Dkt. Biteko amesema Serikali itahakikisha inaweka mazingira
wezeshi ili kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa mizigo kuingia
nchini kutokana na taratibu za forodha. Aidha amesisitiza kuwasilisha
changamoto hiyo katika mamlaka husika.
Kwa
upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Metallica Commodities
Corp, Glendon Archer amesema kiwanda hicho kitawezesha kuboresha maisha
ya wananchi katika maeneo hayo na kuongeza Pato la Taifa.
Pia, ameahidi kushirikiana na Serikali katika kipindi chote cha uzalishaji ili manufaa ya kiwanda hicho yabaki nchini.
Archer
amemshukuru Dkt. Biteko kwa ushirikiano anaopatiwa na Wizara ya Madini
katika kila hatua ili kuweza kujenga kiwanda hicho na kuanza uzalishaji.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Mpakate,
amesema kiwanda hicho kitaongeza fursa mbalimbali kwa wananchi na
Serikali.
Ameongeza
kuwa, wawekezaji hao wa madini ya Shaba watatoa ajira na kuboresha
miundombinu ya maeneo hayo hususan kwa wakazi wa Tunduru.
Kampuni ya Mineral Access System Tanzania Limited pia inatarajiwa kuwekeza kwenye madini ya Lithium na Nikeli nchini.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Metallica Commodities Corp. Glendon Archer akizungumza na Dkt. Biteko kuhusu uwekezaji wa madini ya Shaba leo Agosti 16, 2022 Jijini Mwanza |
Dkt. Biteko akizungumza na wawekezaji wa Kampuni ya Mineral Access System Tanzania Limited Jijini Mwanza |
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza na
wawekezaji wa madini ya Shaba alipokutana nao wawekezaji hao leo Agosti
16, 2022 Jijini Mwanza |
0 Comments:
Post a Comment