Home »
» MTAKWIMU MKUU ASILIMIA 99.93 WAMEHESABIWA NCHI NZIMA
MTAKWIMU MKUU ASILIMIA 99.93 WAMEHESABIWA NCHI NZIMA
Na. Kadala Komba Dodoma
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema tangu kuanza kwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 Mwaka huu Nchini kote hadi kufikia Leo kiwango Cha Kaya zilizohesabiwa imefikia asilimia 99.93na zimebaki asilimia 0.07 tutaendelea kuhesabu Hadi tarehe 5 Septemba 2022.
"Ambapo simu zilizotolewa zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa kwa kuwa utaratibu maalumu ulishaandaliwa wa namna ya kuzifikia Kaya hizo kupitia viongozi wa mitaa na vitongoji.
Dk Chuwa ameyaeleza hayo Leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na zoezi hilo ambalo linamalizika rasmi kesho.
Katika hatua nyingine amesema kuwa Sensa ya Majengo Hadi leo asubuhi tarehe 31Agosti, 2022 jumla ya majengo yaliyokwisha hesabiwa ni 6,351,927 Ambapo taarifa za umiliki,mahali yalipo na taarifa nyingine zinazoanisha katika Dodoso la majengo zimekusanywa.kwa makadirio ni kufikia Majengo Milioni 12.
Aidha Dk.Chuwa amesema kama mnavyofahamu ,Sensa kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 imefanyika Sensa ya watu na makazi (Traditional Census) ya kidigitali ambayo imejumuisha Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi katika mfumo wake wa utekelezaji .
"Alisema Ubunifu huu umeongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama ya kufanya mazoezi makubwa matatu ya kitaifa endapo yangefanyika katika kipindi tofauti.
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari
0 Comments:
Post a Comment