Home »
» JINSI YA KUEPUKA KUCHELEWA KANISANI
JINSI YA KUEPUKA KUCHELEWA KANISANI
1. Piga pasi nguo zako zote kabla ya kulala.
2. Safisha na andaa viatu kabla ya kulala.
3. Tayarisha Biblia yako, Notebook, Kalamu, n.k mahali pamoja.
4. Tayarisha zaka na sadaka yako.(Kisha sema na Mungu unataka akufanyie nini kupitiahiyo sadaka)
5. Lala mapema.
6. Amka kwa wakati ikiwezekana tegesha alarm
7. Epuka kusema "Hata nikifika mapema, sitakutana na mtu yeyote"
Fika mapema na acha mtu aje akukute pia. Usisahau kwamba wewe pia ni mtu.
8.Iwapo itakuchukua dakika 15 kuendesha gari/kutembea hadikanisani, sikuzote toa muda wa ziada kwa kuwa lolote linaweza kutokea. Kwa mfano, ikiwa ibada itaanza
saa 1:00 asubuhi na inakuchukua dakika
10 kuendesha gari/kutembea hadi kanisani, ni bora kila mara kuondoka nyumbani saa 12:40 asubuhi.
9.Panga kufika kanisani angalau dakika30 kabla ya ibada kuanza.
10.Usitoe nafasi kwa marafiki na jamaa kukutembelea saa chache kabla ya Ibada. Ikiwa wanakuja wakati unajiandaa kwenda Kanisani, nenda Kanisani pamoja nao au wafanye wakungojee hadi urudi. Wao si muhimu zaidi kuliko Mungu.
🟩Kwenda kanisani mapemakunaleta baraka za Bwana juu ya maisha yako.
🟩Usiwe na mazoea ya kuchelewa kufika kanisani, ni aibu kwa Mungu wako.
🟩 Kuchelewa kanisani ni kukosa nidhamu kwa aliyekuumba(Mungu)
0 Comments:
Post a Comment