Home »
» Waziri Simbachawene amshukuru Rais kwa fedha ya miradi maendeleo
Waziri Simbachawene amshukuru Rais kwa fedha ya miradi maendeleo
Na.Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha billioni 16 kwa mwaka uliopita wa fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mpwapwa.
Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. George Simbachawene katika mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa. Wenye kauli Mbiu “sensa ni Msingi wa Mpango wa maendeleo. Shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya Taifa.”
“Watu wanahitaji kusikia shida zao zinazungumzwa, ni imani yangu kwamba viongozi tutaendelea kushirikiana na fedha yoyote ya mradi wa maendeleo itakayokuja tutaitumia vizuri”
Waziri Simbachawene amepongeza timu ya wakimbiza Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanya kazi nzuri. Mwenge wa uhuru umekimbizwa kwa umbali wa km 100 na umezindua miradi miwili, miradi mingine miwili imewekwa jiwe la msingi na mradi mmoja kutembelewa yenye thamani ya zaidi billion 1.4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (Kulia) akiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipata juice katika banda la lishe Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bwn. Sahili Geraruma akikagua barabara ya lami Km 1 Mpwapwa mjini kabla ya kuizindua.
Related Posts:
CHAMWINO YAJIWEKEA MPANGO MKAKATI WA KUONDOA ZIRO MASHULENINa Peter Mkwavila CHAMWINO. MKUU wa wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Gift Msuya amesema kuwa ili kuepukana na ziro shule za masingi na sekondari wamejiwekea mpango mkakati wa kuwasaka watoto wasioenda shule na ikiwemo na k… Read More
JINSI YA KUEPUKA KUCHELEWA KANISANI 1. Piga pasi nguo zako zote kabla ya kulala. 2. Safisha na andaa viatu kabla ya kulala. 3. Tayarisha Biblia yako, Notebook, Kalamu, n.k mahali pamoja. 4. Tayarisha zaka na sadaka yako.(Kisha sema na Mungu unataka akufanyi… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 18, 2022… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 17, 2022… Read More
NBS IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI YAONGEZEKA HADI ASLIMIA 62.7. Na.Kadala Komba Dodoma OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema kuwa idadi ya watalii walioingia nchini kuanzia Januari hadi Julai yaongezeka hadi kufikia 742,133 ikilinganishwa na 456,266 kwa kipindi Cha mwaka 2021, saw… Read More
0 Comments:
Post a Comment