Home »
» MCHUNGAJI CHARLES PROSPERITY KUHESABIWA HAKUNA MAHUSIANO NA MAMBO YA GIZA KISHETANIWA YA USHETANI
MCHUNGAJI CHARLES PROSPERITY KUHESABIWA HAKUNA MAHUSIANO NA MAMBO YA GIZA KISHETANIWA YA USHETANI
Na. Kadala Komba Dodoma
MCHUNGAJI kiongozi Charles A. Prosperity wa kanisa la The Covenant Place lililopo kisasa Relini Dodoma amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ya watu na makazi ambalo linatalajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma wakati Mchungaji Charles akizungumza na Waandishi wa Habari umuhimu wa Sensa ya watu na makazi amesema lengo ni kujua watu na makazi yao na mambo mbalimbali ni muhimu Sana ili Serikali iweze kupanga Mipango ya Maendeleo.
“Jambo hili ni jambo la kimaandiko kabisa, kuhesabiwa ni jambo ambalo halijaanza leo ni jambo la kimaandiko tunaona likitajwa kwaiyo naomba nichukue fursa hii kuwahasa watanzania tumuunge mkono mama yetu Samia Suluhu Hassan na pia kuunga mkono jitihada za serikali amesema.
Amesema Kuhesabiwa hakuna mahusiano na mambo ya giza wala ya ushetani, kuhesabiwa ni mahesabu tu na kama tunataka tuendelee tuwe na mahesabu.
Sambamba na hilo Mchungaji Charles Ametolea mfano kwa kabila la Wachaga wanasema MALI BILA DAFTARI HUPOTEA BILA HABARI kwaiyo kama wanataka kuweza kuwa na mali kesho, ni vyema waweze kufanikiwa kesho lazima kuwa na daftari la kujihesab.
"Mambo muhimu tunayaona katika maandiko tunaona katika kipindi cha Musa, kipindi cha kina Adam huko nyuma watu walikuwa wanahesabiwa, watu walikuwa wanaidadi lakini Zaidi kabisa katika habari ya maandiko yetu matakatifu katika kitabu cha LUKA 2 kwamba watu walihesabiwa , kitabu cha [Luka2:1] anasema “siku zile amri ilitolewa kutoka kwa Kaisali Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
Maandiko hayo yanaendelwa kusema orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo kirenio alipokuwa liwali wa shamu. Watu wakaenda kuandikwa , kila mtu mjini kwao” watu wakaenda kuandikwa unaweza ukasema walienda kuhesabiwa kila mtu mjini kwao.Ameaisitiza
Hata hivyo ametoa wito watu kwenda kuhesabiwa kila mmoja lakini na kwa washirika wote wa covenent, wakristo wenzangu wote na waislam na kila mmoja Sensa nikwaajili ya maendeleo ya taifa twende tukahesabiwe Mungu akubariki .
MCHUNGAJI kiongozi Charles A. Prosperity wa kanisa la The Covenant Place
Related Posts:
WALIOITWA KWENYE USAILI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA BAHI PART 1 … Read More
Naibu Waziri Ummy, Apokea jedwali la uchambuzi la Sheria Ndogo Na Mwandishi wetu- DODOMANaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge … Read More
INEC, VYAMA VYA SIASA KUANDAA KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI Na Mwandishi wetu- Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushauriana na vyama vyote vya siasa itaandaa… Read More
JKT HATUTOI AJIRA TUNATOA MAFUNZONa. Kadala Komba Dodoma .JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira.Kaimu Mkuu wa Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai a… Read More
UCHAGUZI MWAKA 2024\2025 UMEWAKUTANISHA WADAU WA SIASA NA VIONGOZI WA DININa. Kadala Komba Bahi Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi,kuanzia hatua ya kujia… Read More
0 Comments:
Post a Comment