Home »
» WACHUNGAJI WATAKA KIGOGO EAGT ACHUNGUZWE
WACHUNGAJI WATAKA KIGOGO EAGT ACHUNGUZWE
NA WAANDISHI WETU.
Baadhi ya Wachungaji waKanisa la The Evangelistic Assemblies of God Tanzania(EAGT), wameutaka uongozi wa juu wa kanisa hilo kumchunguza na kumchukulia hatua ikibidi, mmoja wa Wadhamini wa kanisa hilo, Mchungaji Dkt. Kenneth
Kasunga kutokana na kile ambacho wamesema “amekosa uaminifu” kama anavyotakiwa na Katiba ya EAGT.Katika taarifa yao waliyoituma kwa gazeti la MWANZO wiki hii,wachungaji hao ambao wameomba majina yao
yasiandikwe, wameeleza kuwa kuna mambo
mawili ambayo kanisa linapaswa kuyatumia ili kumchunguza Dkt. Kasunga.Jambo la kwanza, wachungaji hao wanadai, Dkt.Kasunga ambaye huchunga Kanisa la EAGT Kyela mjini mkoani Mbeya, ameharibu imani ya umma kwa EAGT kimafundisho kutokana na kutetea mahubiri yasiyo sahihi kulingana na Kurugenzi
ya TEBE ambayo husimamia mafundisho na uinjilisti katika kanisa hilo.
Jambo la pili, wachungaji hao wanadai, mchungaji huyo alishindwa kusimama katika misingi ya kiuongozi na kusababisha waliokuwa viongozi wa EAGT Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kati kujiuzulu. Wanadai mchungaji huyo alifanya kitendo ambacho baadaye kilisababisha madhara hata kwa viongozi wakuu wa EAGT.Wakifafanua katika taarifa yao hiyo, Wachungaji hao wanadai kuwa kitendo cha Mchungaji Dkt. Kasunga
kumtetea, kumlinda na kuchukua mafungu ya kumi kutoka kwa mwanamke anayehubiri ‘injili iliyojaa simulizi za uchawi’ ambayo imepingwa na Kurugenzi ya TEBE pamoja na walimu wa Biblia, inatia shaka uaminifu wake.
Wiki iliyopita, Dkt. Kasunga aliliambia gazeti hili katika mahojiano kuwa, yeye hana shida na anaikubali injili ya simulizi za uchawi inayohubiriwa na mwanamke anayejulikana kwa jina la Josephine Thobias.MWANZO lilimtafuta Dkt. Kasunga baada ya Josephine kudai kuwa amehamishia mafungu yake kwa Mdhamini huyo wa EAGT baada ya kujiondoa kwa aliyekuwa Askofu wa EAGT Kanda ya Mashariki, Mchungaji Dkt.Nicodemus Nyenye. Dkt. Nyenye huchungaji kanisa la EAGT Patmo, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mwanamke huyo alisema Dkt. Kasunga ndiye amekuwa mlezi wake. Mazungumzo baina ya MWANZO na Dkt. Kasunga ambayo yalikabiliwa na kizuizi baada ya awali kugoma kuzungumza akidai kuwa gazeti limewachafua viongozi wa EAGT kwa kuchapisha habari bila kuwauliza, akiwemo yeye.
Related Posts:
WAPIGA KURA 74,642 KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO Na Mwandishi maalum - NECWapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.Jumla ya w… Read More
WANANCHI WAALIKWA MIAKA 60 YA JKT Na Moreen Rojas,Dodoma.Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa amewaalika wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yatakayofanyika tarehe 10 julai siku ya jumatatu … Read More
SERIKALI HAIPO TAYARI KUMPOTEZA MTU Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Serikali haipo tayari kuona Mwananchi yeyote anapoteza uhai wake kwa sababu za ama ujambazi au udereva mbovu barabarani au migogoro ba… Read More
BAHI KINARA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA BOOST Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe madarasa 51, Vyoo 63 na nyumba 1 ya waalimu ikiwa ni sawa na shule 7 zilizokamilika katika Wilaya ya Bahi. Ak… Read More
HUAWEI AT MWC SHANGHAI 2023:BOOSTING 5G EVOLUTION TOWARDS 5.5G REVITALIZE THE DIGITAL ECONOMYHuawei has shown up in full force for MWC Shanghai 2023, with their activities all falling under their theme of "GUIDE to the Intelligent World". This year, the company's activities include an experiential tour that takes aud… Read More
0 Comments:
Post a Comment