Home »
» ASKOFU DKT. MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU
ASKOFU DKT. MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU
NA. MWANDISHI WETU.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 nchini.
Ametoa kauli hiyo wakati akihubiri kwenye ibada ya jumapili tarehe 21 Agosti, 2022 katika kanisa lake la EAGT Mlimwa West lililopo Maili Mbili Jijini Dodoma.
Askofu Mwakipesile alisema ni jukumu la kila muumini kuwa kielelezo kizuri katika jamii kwa kuwa tayari na kuonesha ushirikiano kwa makarani wa sensa ili kufanikisha zoezi hilo.
“Kila aliyeokoka awe mfano kwenda kuhesabiwa, popote alipo mwana EAGT ahakikishe anakuwa mstari wa mbele kushiriki zoezi la sensa,”alisema Dkt. Mwakipesile.
Aliongezea kuwa, sensa ni jambo muhimu kwa kuzingatia idadi ya watu inahitajika kila eneo ikiwemo katika kanisa ili kufanishi mipango ya maendeleo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile
Related Posts:
CHUO KIKUU HURIA NDIO CHUO KINACHOTENGENEZA WATU WENYE UWEZO. Na Moreen Rojas,Dodoma.Chuo kikuu huria(open university) ndio chuo kinachotengeneza watu wenye uwezo kwani watu wanaosoma huku asilimia kubwa wanauwezo wa kuchanganua changamoto mbalimbali.Hayo yameelezwa na Mhe.George … Read More
*Tume yatangaza matokeo Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara*Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali, Bw. Missana Kwangura amemtangaza Bi. Bahati Ndingo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 44,334 kati ya kura 56,095 halali z… Read More
Naibu Waziri Nderiananga akutana na kufanya mazungumzo na RC Morogoro Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Programu ya Ku… Read More
SACP MISIME AWATAKA ASKARI POLISI KUBADILIKA KIFIKRA NA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI Na, Benedict Mlawa wa Jeshi la PolisiMsemaji wa Jeshi la Polisi Nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) David Misime amefunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa,Wakaguzi na Askari wa Polisi ku… Read More
*GEITA TUPO NJIANI UWT MOTOO MOTOO**ZIARA YA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA BARAZA KUU LA UWT PAMOJA NA WAJUMBE WA NEC MKOA WA GEITA*Ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Mary Chatand… Read More
0 Comments:
Post a Comment