Subscribe Us

WAZIRI MASHIMBA NDAKI SERIKALI IMETENGA SH. BILLIONI 60 KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI

Na.Kadala Komba Dodoma SERIKALI imetenga sh.bilioni 60 kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuboresha shughuli zao, kuwaongezea mitaji na kuwapatia ajira ya uhakika. Hayo yamejili leo jijini Dodoma, na Waziri wa Uvuvina Mifugo Mashimba Ndaki wakati wa hafla ya kusaini makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi,vizimba vya samaki. “Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza wizara kuhakikisha kuwa uzalishaji wa samaki unaongezeka kutoka tani 497,567 na kufikia tani 600,000 ifikapo mwaka 2025. Aliongeza kuwa :”Kwa kuona fursa hiyo na kwa kuzingatia maelekezo na maagizo hayo katika mwaka 2022/2023 serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vyama vya ushirika, vikundi vya wavuvi, wakuzaji viumbe maji, wavuvi binafsi na makampuni ya wavuvi. Waziri alisema mikopo hiyo itahusisha zana za kisasa za uvuvi ikiwemo boti, nyavu, injini, vizimba, vifaranga vya samaki, chakula cha samaki na pembejeo za ukulima wa mwani. Ndaki alisema wizara ya mifugo na uvuvi kupitia sekta ya uvuvi watahakikisha kuwa mikopo hii inawafikia walengwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa ili kuongeza uzalishaji na kuongeza mchango wa Sekta ya Uvuvi kwenye pato la Taifa. “Natoa wito kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji kutumia mikopo hii kama ilivyokusudiwa na kuirejesha kwa wakati ili mkopo huu uweze kuwanufaisha wengine na kuwa endelevu. Sote tunafahamu kuwa, Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini. Alisema Kwa takwimu zilizopo, zaidi ya wananchi milioni 4.5 wameendelea kupata mahitaji yao kutokana na shughuli zinazohusiana na Sekta ya Uvuvi. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo (Uvuvi) Dk.Rashid Tamatama alisema serikali imekuja na mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuvikopesha vyama vyaushirika, vikundi vya wavuvi, wavuvi binafsi na makampuni ya wavuvi. Alisema watakopeshwa seti iliyotimia ya boti zenye urefu wa mita 7 hadi 14 zikiwa na injini zenye uwezo wa nguvu za farasi 9.9 hadi 60. Dk, Tamatama alisema boti hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba wavuvi sita hadi 20, kubeba Samaki tani 1.5, mtambo wa kufuatilia/kutambua uwepo wa Samaki , kifaa cha kuongoza boti , vifaa vya kuokolea Maisha na zana za uvuvi zikijumuisha mishipi na nyavu. “Jumla ya sh.bilioni 11.5 zitatolewa kwa ajili ya zimetengwa kwa ajili ya kukopeshwa na utalipwa kwa muda wa miaka mitano bila riba.pamoja na mkopo wa boti, Wizara pia itatoa mkopo kwa wafugaji samaki kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kujenga jumla ya vizimba 831 ambapo kila kizimba kimoja kitakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 144 M 3 – 256 M 3 . Katika hatua nyingine alieleza kuwa serikali itatoa vifaranga 4,080,000 na chakula cha Samaki tani 3,482.5. Aliongeza kuwa mkataba huo unaosainiwa utahusisha wakulima wa mwani ambapo wakulima 821 watakopeshwa kamba 108,372, tai tai 7,152,552 pamoja na mbegu za mwani. “Kwa ujumla kiasi cha sh.bilioni 21 zitatumika kwa ajili ya vizimba na zao la mwani,”alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki yak Maendeleo yak Kilimo (TADB) alisema watahakikisha mikopo hiyoinawafikia walengwa nakutoa matokeo chanya ya kuongeza mazao yatokanayo na uvuvi. “Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha hizi nyingi ambazo zinaenda kuwagusa wavuvi wa chini na kati na katika kuhakikisha mikopo yak fedha hiyo inatolewa kwa walengwa tumejipanga kuhakikisha inaenda kuwanufaisha,”alieleza Awali akitoa salamu za Bunge Mwenyekiti wa Kamati yak Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dk. Christine Ishengoma alisema kamati hiyo inampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuinua sekta ya uvuvi nchini. Alisemakatika kuhakikisha fedha hizo zinatumika pasipo ubadhilifu watahakikisha wanawatembelea mara kwa mara walengwa ili kuangalia namna mikopo hiyo itakavyo wanufaisha.
Waziri wa Uvuvina Mifugo Mashimba Ndaki wakati akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezajiwakati akizunguma katika
Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo (Uvuvi) Dk.Rashid Tamatama akitoa Utambulisho na Lengo la hafla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine akitoa neno la shukrani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha hizi nyingi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais - TAMISEMJ Dkt. Grace Magembe.
Mwenyekiti wa Kamati yak Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dk. Christine Ishengoma akitoa salamu za Bunge.
Matukio mbali mbali wakati kusaini mkataba wa makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi,vizimba vya samaki.
Picha ya pamoja makundi mbali mbali

0 Comments:

Post a Comment