Home »
» Watendaji wahimizwa kuongeza kasi utekelezaji wa Mradi wa AFDP
Watendaji wahimizwa kuongeza kasi utekelezaji wa Mradi wa AFDP
Na Mwandishi wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza kuwa na vikao vya uratibu vya pamoja kati ya wizara na taasisi zinazotekeleza mradi wa mradi wa AFDP ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es salaam ambalo linatekeleza programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi katika mradi wa AFDP unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu na kutekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Zanzibar.
Waziri Smbachawene amesema programu AFDP ni ya miaka sita kuanzia 2021/2022 hadi 2027/2028 ambayo itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani 77.4 millioni (Mkopo toka IFAD USD 58.8 millioni; Serikali USD 7.7 millioni; Sekta Binafsi 8.4 millioni na Wananchi USD 2.4 millioni).
“Mradi huu wa uchumi wa bluu ukisimamiwa vizuri utaibua shirikia la TAFICO, na utaibua uchumi wa biashara ya uvuvi zinazofanywa na sekta binafsi. “
Lazima tutengeneze kikosi kazi kitakachokuwa kinaashughulikia changamoto zinazojitokeza kutoka taasisi moja kwenda nyingine pamoja na wizara moja kwenda nyingine katika utekelezaji wa mradi, alisema Waziri.
“Eneo hili linaloshughulikiwa na shirika la TAFICO linaenda kujibu ahadi za ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.”
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema mradi huu ni mradi mkubwa sana na ni mradi wa kimkakati.
“Tuone namna ambavyo tutautekeleza huu mradi kikamilifu, spidi na kazi ya utekelezaji wa mradi bado hairidhishi.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shirika la TAFICO Profesa Yunus Mgaya amesema wanalichukulia shirika la TAFICO kama shirika la kimkakati hasa katika dhana ya kutekeleza uchumi wa blue.
“Shirika linajukumu la kuwasaidia wavuvii wadogo wadogo hasa katika kunyanyua vipato vyao, kuwawezesha kuhifadhi mazao yao ya uvuvi kuingia ubia na wananchi mbalimbali katika shughuli za uvuvi bahari kuu”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na watendaji wa shirika la uvuvi Tanzania (TAFICO) alipotembelea kupokea taarifa ya mradi wa kuendeleza kilimo na uvuvi (AFDP)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao na watendaji wa TAFICO.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TAFICO Bi, Esther Mulyila akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene vifaa vya shirika katika Gati la TAFICO lilopo kigamboni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akitazama eneo la Gati la TAFICO.
Related Posts:
BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO NCHINI [CPB] IMEWATOA HOFU WAKULIMA WA MAZAO YA KUNDE Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE … Read More
UZINZI NA UASHERATI NI VYANZO VYA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE MAISHA YA MTU“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.Waebrania 13:4 Siku zote mtu hutumikia adhabu ya kifungo na yapo madhara makubwa yatokanayo na vifungo vya… Read More
SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA ULINZI NA UFUATILIAJI MIENENDO YA WANYAMAPORI Na. Mwandishi wetu MorogoroSerikali Kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kutumia teknolojia ya kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika maeneo ya hifadhi kwa kuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kut… Read More
WAZIRI WA SHERIA DKT DAMAS NDUMBARO AMETOA UFAFANUZI KUHUSU WANAFUNZI WA SHERIA KUFELI MAFUNZO KWA VITENDONa. Kadala Komba Dodoma Kumekuwa na sintofahamu kuhusiana na matokeo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST), mjadala ulioibuka katika sehemu mbalimbali kwamba kwa … Read More
MIAKA 7 YA BMH: MKURUGENZI AELIMISHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE Na. Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Hospitali ya Benjamin MkapaHospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo Oktoba 13, imetimiza miaka saba tangu ilipoanza kutoa huduma za Afya Oktoba 13, 2015. Mkurugenzi Mtendaji D… Read More
0 Comments:
Post a Comment