Home »
» JIFUNZE KUHUSU MTI UNAFUNDISHA MENGI
JIFUNZE KUHUSU MTI UNAFUNDISHA MENGI
Na.Mwl Triple J.
"Basi *KWA MTINI JIFUNZENI* mfano; *TAWI LAKE likiisha KUCHIPUKA NA KUCHANUA MAJANI* , mwatambua ya kuwa *WAKATI WA MAVUNO U KARIBU"*(Mathayo 24:32)
...MAISHA Ya MWANADAMU ni Kama MTI, Matendo Yake ndiyo *MATUNDA Yake.*
...Yaani *MTI ni WEWE* na MATUNDA Ndiyo *Matendo Yako.*
....YESU anasema *KWA MTINI TUJIFUNZE*....JE TUNA YAPI YA KUJIFUNZA....?.
*1. MTI KADRI MTI UNAVYO KUWA MKUBWA NDIVYO HUZIDI KUZAMISHA MIZIZI YAKE CHINI ZAIDI.*
...Usikubali *Kubaki Juu Juu Kila Siku, Kadri Unavyozidi Kukua Kiroho Zamisha IMANI Yako Kwa Mungu Zaidi.*
...Komaza Mizizi ya IMANI Yako, *Usije Kuangushwa Na Ghassia , Mvua Na Upepo Wa Shetani.*
.....MWANADAMU Jifunze pia Kadri MUNGU anavyokuinua endelea Kunyenyekea Chini Zaidi.
*(1 Petro 5:6).*
*2. KILA MTI UNA KAZI YAKE MAALUMU.*
- 🥦Mfano, Mti Wa Mwembe, Mpera, na Mparachichi *HUWEZA KUTENGENEZA JUICE, n.k Lakini Kuna Miti HAIWEZI.*
-🥦Mfano ,MWAROBAINI Hauwezi hiyo kazi , *Lakini Una Kazi Yake Maalum Kama KUJIFUKIZA na KUTIBU baadhi Ya Magonjwa.*
-🥦NDIVYO alivyo Mwanadamu Tupo kila Mmoja kutimiza Kazi Maalum Hapa Duniani, *Huyu Mwalimu, Huyu Daktari, Huyu Seremala , Huyu Mkulima na Huyu Padre (Mchungaji), PLAY YOUR PART Vizuri.*
-🥦Hakuna MTI uliopo Tu Ardhini Hauna Kazi , Hivyo Tambua pia *Hakuna Mwanadamu Aliyekuja Kuzurura Duniani.*
*3. KUPIGWA MAWE NI SEHEMU YA MAISHA YA MTI.*
...Mti Hupigwa Mawe Kwa Kile Ulichobeba Kiwe Kizuri Au Kibaya.
...Mti Ukibeba Matunda *UTAPIGWA tu.*
...Mti Hata Ukibeba Nyoka *UTAPIGWA pia.*
....Tambua kuwa MWANADAMU Vile Vile UTAPIGWA Mawe Kwa Njia Yingi *(Maneno, Masengenyo, Chuki, Wivu , n.k.).*
....LAKINI KUMBUKA *siyo KILA MTI Upigwao Mawe Una Matunda NO, Miti Mingine Hupigwa Kwa Sababu Ina NYOKA.*
...Wewe Hayo MAWE Upigwayo , *Je Umebeba MATUNDA au NYOKA ?.*
*4. MTI HUPITIA NA KUVUMILIA NYAKATI MBALIMBALI.*
...Kuna Wakati Mti *HUPUKUTISHA MAJANI na Kupoteza Uzuri wake.*
...Huvumilia MVUA Kali Zenye UPEPO.
...Huvumilia *Wakati Wa JUA KALI kiasi cha kupoteza MAUA yake.*
....MWANADAMU Jifunze *Kuvumilia NYAKATI na MAPITO magumu,* Hayadumu Milele ni ya Muda tu .
...Taabu, Masumbuko, Maumivu, Mateso , Dhiki n.k *Yapo kukuimarisha VUMILIA.*
....Jifunze *KUWA RADHI* Kwa HALI ZOTE.
*5. MTI MZURI HUTOA KIVULI NA HEWA SAFI KWA MAPUMZIKO.*
....MWANADAMU *Jifunze Kuwa Sehemu ya Faraja, Upendo , Amani , Kitulizo, na Furaha Kwa Watu Wanaokuja Kwako Kuhitaji Msaaada wako.*
....Uwe Sehemu Ya MAISHA Yao , Kuwa Mtu Mwema Na Unayegusa Maisha Ya Wengine kwa Upendo .
*6. MTI NI DAWA, HUTIBU NA KUPONYA.*
...Miti Hutibu Na Kuponya Magonjwa.
...Hivyo *Usikubali Kuwa Chanzo Cha Ukosefu Wa FURAHA na Afya* Kwa Wengine Kiroho Na Kimwili.
..Bali Jifunze Kuponya Majeraha ya Walioumizwa.
...Tuliza *MIOYO ILIYOPONDEKA.*
-Fariji Na Kuwa tia Moyo *WENYE HUZUNI.*
*7. KILA MTI HUZAA KWA MAJIRA YAKE.*
...Miti Huwa ni Tofauti, *Kila Mti una majira Yake Ya Kustawi Na Kuzaa Matunda.*
...Ndivyo Tulivyo WANADAMU *Kila mmoja hustawi Kwa Wakati wake na Majira Maalum.*
...Usijione Umechelewa Kwenye Jambo Fulani *Tambua Tu Kuwa Majira Bado.*
*8. MTI BILA ARDHI HUKAUKA NA KUFA.*
...Kwani Ardhini ndiko Mti utoako na Kujipatia *Maji Na Chakula Chake.*
...Ndiko Mizizi Yake inapata Support ya Kuweza Kusimama.
*....TUTAMBUE Na KUFAHAMU* Kuwa Maisha Yetu Bila Mungu tutaangamia Na Kupotea kama si Kufa .
...MUNGU ndiye Uhai na Uzima wetu *.Ni Yeye atupaye Pumzi, Chakula ,Maji Na Afya.*
...Yatupasa Kudumu Nyumbani Mwa Bwana Daima.
Lakini *KUMBUKA....*
"...SHOKA limekwisha kuwekwa penye mashina ya Miti; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA mazuri hukatwa na kutupwa MOTONI" (Math 3:10)
Mwenye Masikio Na Asikie.
Related Posts:
NAIBU WAZIRI MERYPRICA MAHUNDI AMETOA OYO KALI KWA WALE WANAOCHEPUSHA MAJI Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wanan… Read More
TANROADS YATUMIA SHILINGI TRILIONI 1.37 KUKAMILISHA MIRADI 14 KWA KIPINDI CHA SERIKALI AWAMU YA SITA.Na Moreen Rojas, Dodoma Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania … Read More
WAZIRI SIMBACHAWENE, AMPONGEZA MAMA TUNU PINDANa Mwandishi wetu Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa. Kauli hiyo imetolewa na W… Read More
UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KULETA TIJA KWA WATANZANIANaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amebainisha kuwa, biashara ya Makaa ya Mawe inatarajia kuleta tija kwa Watanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo ndani na nje ya nchi. Dkt. Kiruswa ameeleza hayo Novemba… Read More
RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA NA MUONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO HAYO JIJINI DODOMANa. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo … Read More
0 Comments:
Post a Comment