Home »
» *MAMBO MHIMU YA KUOMBA PINDI UNAPOKUWA NYAKATI NGUMU AMBAZO HAUJUI UTAFANYA NINI..*
*MAMBO MHIMU YA KUOMBA PINDI UNAPOKUWA NYAKATI NGUMU AMBAZO HAUJUI UTAFANYA NINI..*
Sehemu ya kumi.
*11. Omba Mungu yakwamba maneno ya kinywa chako na mawazo yako yapate kibali mbele zake.*
Biblia inasema hivi👇🏻
*👉Zaburi 19:14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.*
👆🏻Kwenye haya maandiko mtunga zaburi anamwomba Mungu yakwamba MANENO YA KINYWA CHAKE na MAWAZO YAKE yapate kibali mbele za Mungu, kwanini akaomba maneno na mawazo yake yapate kibali kwa Mungu? Ni kwasababu alijua yakwamba mwenye ufunguo wa kufanikiwa kwa maneno ya kinywa chake na mawazo yake ni Mungu peke yake, kama ni hivyo hata wewe hasa unayepita nyakati za mapito hivi sasa jifunze kumwomba Mungu yakwamba MANENO YA KINYWA CHAKO na MAWAZO YAKO yapate kibali mbele zake.
*✅Ni hivi nyakati za mapito yako unaweza ukawa na mawazo mengi mazuri ya kukufanikisha kimaisha lakini kama mawazo yako hayatapata kibali mbele za Mungu hayawezi kukusaidia chochote, ndiyo maana nilazima ujifunze kwenda mbele za Mungu na kumwambia EE MUNGU NINAKUOMBA MAWAZO MAZURI NILIYONAYO HIVI SASA YAPATE KIBALI MBELE ZAKO, ni hivi mawazo yako yakipata kibali kwa Mungu uwe na uhakika ni rahisi mawazo hayo kukufanikisha kimaisha..*
✅Inawezekana sasa hivi uchumi wako si mzuri ila una mawazo mazuri na mema ya jinsi unavyoweza kupata Pesa nasema hivi yapeleke hayo mawazo mbele za Mungu, Mwambie Mungu ninaomba mawazo yangu yapate kibali mbele zako utashangaa namna Mungu atakavyo kufanikisha...
*✅Inawezekana umesoma lakini haujapata ajira, na kinywani mwako una maneno mazuri ya kitaaluma ya kuyashawishi makampuni ili yakupe ajira nasema hivi nenda mbele za Mungu mwambie Mungu yakwamba maneno ya kinywa changu ninaomba yapate kibali kwako, ni hivi maneno yako yakipata kibali kwa Mungu hata hiyo kampuni itayokuita kwenye interview ili upewe ajira nayo itayakubali maneno yako na kukupa ajira USIOGOPE!*
✅Inawezekana kuna binti unampenda na unatamani kumwoa lakini unajiuliza hivi nikimwelezea hisia zangu kwake atanielewa kweli? Nasema hivi omba kibali kwa Mungu, maneno yako yakipata kibali kwa Mungu hata kwa huyo binti yatapata kibali USIOGOPE...😊
✅️Inawezekana una mawazo ya kujenga, mawazo ya kununua kiwanja, mawazo ya kuanzisha biashara fulani n.k nasema hivi yapeleke hayo mawazo yako kwa Mungu, mawazo yako yakipata kibali kwa Mungu uwe na uhakika yatakufanikisha kimaisha...
*✅Inawezekana binti umri unaenda na haujaolewa na unatamani ujao wa 2023 na wewe ukavae shera lako, nasema hivi nenda mbele za Mungu mwambie Mungu yakwamba NINAOMBA MAWAZO YANGU YA KUOLEWA MWAKA HUU TUNAOKWENDA KUUANZA YAKAPATE KIBALI MBELE ZAKO BWANA, utashangaa 2023 jinsi itakavyokuwa mwaka wako wa shangwe na furaha kwenye maisha yako...*
▶️Narudia tena, inawezekana una mawazo mengi mazuri kwa habari ya maisha yako, yapeleke mbele za Mungu hayo mawazo yako na hayo mawazo yako yakipata kibali kwa Mungu hakuna kitu chochote cha kukuzuia usifanikiwe kimaisha kwa jina la Yesu..
*✅NASEMA HIVI, HAKUNA MTU WA KUKUZUIA USIFANIKIWE KIMAISHA IKIWA MANENO YAKO NA MAWAZO YAKO YATAPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU, KWAHIYO OMBA WALA USIOGOPE..*
🔳Mwisho..
Ni ombi langu kwa Bwana yakuwa, mawazo yako mema uliyonayo kwa habari ya maisha yako basi yakapate kibali mbele za Mungu kwa jina la Yesu..
*👉Zaburi 106:4 Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako,*
Mungu wa mbinguni awabariki sana🙏🏽
WhatsApp +255657117595
Mwl.Joseph Leonard
0 Comments:
Post a Comment