Subscribe Us

RC SENYAMULE MAANDALIZI YA SENSA YAMEKAMILIKA ASILIMIA 98

Na.Kadala Komba Dodoma MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema ili kuhakikisha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022 linafanyika kwa ufasaha Mkoa wa dodoma umezindua namba maalumu ya simu ambayo kaya yoyote isipofikiwa na karani kuhesabiwa mwananchi atapiga namba hiyo bure. Mwananchi atapiga simu kwa kupitia namba za bure ambazo ni 0800110083 na kueleza mtaa au kitongoji anapoishi na uongozi wa Mkoa utawasiliana na karani aliyepangiwa katika eneo hilo na kufika kuhesabu kaya husika. Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodma leo Agosti 21,2022 Senyamule amesema maandalizi ya sensa yamekamilika kwa asilimia 98 ikiwemo mafunzo kwa makarani, vifaa vya sensa,usafiri na masuala ya kifedha kwa ajili ya kuwezesha zoezi la sensa kufanyika. "Hadi sasa makarani wamesambaa Katika maeneo yao waliyopangiwa kwa ajili ya kujitambulisha kwa viongozi wa maeneo hayo kutambua eneo lake la kuhesabu watu katika eneo lake ambapo Mkoa wa dodoma una jumla ya makarani 10,353 ambao watafanya kazi ya kuhesabu Katika maeneo waliyopangiwa,"amesema Senyamule Ameongeza kuwa"Serikali inawaomba wananchi wote kushiriki zoezi la sensa kuanzia siku ya jumanne kwa kuhakikisha wanashiriki kihesabiwa na wanahesabiwa mara moja tu na wanatakiwa kutambua kuwa ni kosa kisheria kukataa kushiriki zoezi hilo. Senyamule amewataka wananchi kuandaa taarifa za kaya Ili kurahisisha zoezi la sensa ya watu na makazi ,ambapo taarifa hizo ni pamoja na umri wa wanakaya,hali ya ajira,Elimu,taarifa za Kilimo na mifugo namba za kitambulisho cha taifa (NIDA) na namba ya simu ya wanakaya. Pa Senyamule amewataka makarani kuhesabu watu katika eneo lake alilopangiwa kwa ufasaha na kutunza siri za kaya alizohoji na kutambua kazi hiyo inafanyikia kwa maslahi ya taifa Katika kupanga mipango ya maendeleo. "Nitumie fursa hii kuwa sisitiza wakuu wa wilaya wote wa Mkoa wa dodoma kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na Usalama za wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri. kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo Ili lifanyike kwa mafanikio kama ilivyopangwa,"amesema.

0 Comments:

Post a Comment