Home »
» JITOKEZENI KWENYE ZOEZI LA SENSA ILI MUHESABIWE
JITOKEZENI KWENYE ZOEZI LA SENSA ILI MUHESABIWE
Na. Mwandishi Wetu.
Jitokezeni kwenye zoezi la sensa ili muhesabiwe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.
“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla”
Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene baada ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa lile fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.
“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agusti 2022, alisema Waziri”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa anatoa taarifa muhimu kwa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na makarani wa Sensa ya watu na Makazi.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Related Posts:
HUAWEI UNLEASHERS AFRICA'S DIGITAL FUTURE THROUGH FULL UTILISATION OF SUB-3GHZ DURING A BETTER AFRICA SPECTRUM PRACTICE ROUNDTABLE Opening Ceremony: Jacob Munodawafa, Executive Secretary of Southern Africa Telecommunications Association (SATA) ...........(MAPUTO, The critical annual Africa Spectrum Roundtable, one of the continent’s most impor… Read More
WAZIRI WA MAJI AWESO AMETENGUA UTEUZI WA MENEJA WA MAJI MKOA WA DODOMA Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa H. Aweso (Mb) ametengua uteuzi wa Meneja wa Maji Mkoa wa Dodoma, (RUWASA) Mhandisi Godfrey Kabula Mbabaye kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Waziri Aweso amechukua hatua hiyo… Read More
BUI POWER AUTHORITY IMPROVES OPERATIONAL COVERAGE USING HUAWEI ELTE SOLUTION [Accra, Ghana:The International Renewable Energy Agency estimates that Africa’s renewable energy capacity could reach 310GW by 2030, catapulting the continent into the top tier of green energy production. The Bui Power … Read More
KAMATI YA UFUNDI YA SERIKALI MTANDAO YAFANYA KIKAO CHA KWANZA JIJINI DODOMA Kamati ya ufundi ya serikali mtandao imefanya kikao cha kwanza na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha jitihada za serikali mtandao zinaimarika na kuleta ti… Read More
KATAMBI AMEWATAKA WAKURUGENZI WAKUU WA MIFUKO YA PENSHENI KUHAKIKISHA MWANACHAMA ANALIPWA NDANI YA SIKU 60. Na Moreen Rojas,Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe.Patriobas Katambi amewataka Wakurugenzi wakuu wa Psssf na Nssf kuhakikisha kila mwanachama analipwa ndani ya siku 60 z… Read More
0 Comments:
Post a Comment