Home »
» KAMISHNA WA MADINI ATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU
KAMISHNA WA MADINI ATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU
Na.Mwandishi Wetu.
Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga ametembelea Mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga katika ziara iliyolenga kufuatilia shughuli za uzalishaji.
Vile vile Dkt. Mwanga ametembelea maeneo ya machimbo chini ya ardhi (underground) na mitambo ya uchenjuaji (process plant).
Ziara hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kufuatilia shughuli za uzalishaji pamoja na changamoto zinazoikabili Mgodi wa Bulyanhulu na kujua mwenendo wa uzalishaji kwa sasa.
Kamishna alizungumza na uongozi wa mgodi na kusisitiza kuwa wawe karibu na Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake pindi wanapopata changamoto yoyote na wasisite kutoa taarifa.
Pia alisisitiza pindi mgodi unapotaka kufanya manunuzi au kubadilisha mtambo wowote ni vema wakatoa taarifa Tume ya Madini kwa hatua stahiki .
Halikadhalika aliutaka uongozi wa mgodi kufikiria njia bora ya kuhakikisha madini yote yanayozalishwa mgodini yanaongezewa thamani hapa nchini.
Naye, Meneja Mkuu wa Mgodi Cheick Sangare alieleza kuwa mgodi huo upo tayari kushirikiana na Serikali.
Related Posts:
WAZIRI PINDI CHANA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TAWAWaziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo tarehe 12 Oktoba, 2022 amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA aliyoiteua hivi Karibuni.Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya TAWA Mk… Read More
SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWA WATAALAMU WA NDANI WA MIFUMONa WAF - DSMKatibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza kwa Wataalamu wa ndani wa mifumo ili kuhakikisha miradi yote inayoanzishwa na Wafadhili inaendelea kusimama siku Wafad… Read More
WADAU WA MAENDELEO WAHIMIZWA KUCHANGIA VIFAA VYA MISAADA YA KIBINADAMU WAKATI WA MAAFA. Na Mwandishi wetu- Kilimanjaro Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuchangia vifaa vya mi… Read More
WAZIRI WA SHERIA DKT DAMAS NDUMBARO AMETOA UFAFANUZI KUHUSU WANAFUNZI WA SHERIA KUFELI MAFUNZO KWA VITENDONa. Kadala Komba Dodoma Kumekuwa na sintofahamu kuhusiana na matokeo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST), mjadala ulioibuka katika sehemu mbalimbali kwamba kwa … Read More
MCHUNGAJI AWATAKA WAGONJWA WANAONGUDULIKA NA TATIZO LA AFYA AYA AKILI WAPELEKWE HOSPITALI BADALA YA KWA WAGANGA WAKIENYEJI.Na Peter Mkwavila CHAMWINO. ASKOFU wa kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Kanda ya Kati Brayson Msanjila,amewashauri familia zinazogundulika kuwa na wagonjwa wa afya ya akili waac… Read More
0 Comments:
Post a Comment