Home »
» ASKOFU MWAKANDULU MIPANGO YOYOTE BILA TAKWIMU HUKUMU YAKE NI UMASIKINI
ASKOFU MWAKANDULU MIPANGO YOYOTE BILA TAKWIMU HUKUMU YAKE NI UMASIKINI
Na. Kadala Komba Dodoma.
Askofu Emmanuel Mwakandulu wa kanisa la Baptist jimbo la Dodoma mjini amesema Sensa sio jambo la kisiasa hili kujua idadi ya watu unaowaongoza lazima ujue idadi halisi ya watu, bali ni jambo la kibiblia pia katika Biblia kuna kitabu kinaitwa Hesabu kwasababu kuna watu walihesabiwa [Hesabu 1:2-3]Pia katika Agano jipya tunasoma ya kwamba Yusufu na Mariam wazazi wa Yesu waliondoka Galilaya mji wa Nazaleti walienda Bethlehemu kuhesabiwa [Luka :1-5] Wakristo na watanzania msiwe na mashaka na zoezi la sensa ya watu na makazi ni jambo la Baraka alisema pia Yesu aliwalisha watu elfu tano 5,000/= kwa mikate mitano, inaonekana Yesu alifanya miujiza kwakuwa watu walihesabiwa, watu ni wengi mikate ni midogo sana alisema bila Takwimu mujiza wa Yesu usingeonekana.
Askofu Emmanuel Mwakandulu ameyasema hayo alipokuwa anazungumuza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu mchango wa viongozi wa dini katika zoezi la sensa ya watu na na makazi mwaka huu katika ofisi za kanisa hili jijini Dodoma Amesema Sensa ya watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 katika Nchi yetu ya Tanzania. Sensa ya mwaka huu wa 2022 itakuwa Sensa ya 6 kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa zingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.amesema Umuhimu wa kipekee wa sensa ya watu na makazi ni kutaka kujua Takwimu sahihi, ambazo zitaweza kuisaidia serikali katika utekelezaji wa dira ya maendeleo katika maswala ya Afya, kielimu na katika agenda za maendeleo ya kimataifa.
Sambamba na hilo Askofu Emmanuel Mwakandulu ametoa mfano wa Mtaalamu mmoja ambaye alishawahi kusema “utafiti wakina na sahihi na wakina na uliosahihi unaleta taarifa sahihi na taarifa sahihi itaufanya utekelezaji wa maendeleo kuwa sahihi na halisi, amesema Njia mojawapo ya kupima ukuaji wa taifa lolote lile ni kuwa na TAKWIMU sahihi ya watu.
Alisema Kujidhania upo vile ambavyo hauko ni kujidanganya ambako kunaweza kukasababisha anguko kubwa la uchumi badaye,amesema Lengo la serikali ni kutaka kutuhesabu ili kutaka kuwa na idadi halisi ya watanzania, pia ni kutaka kujijua mahali tulipo, na kujua mahali tulipo, na tutajua mahali tunapotaka kwenda hivyo Ndugu watanzania wenzangu watu ndio rasilimali muhimu katika taasisi na katika taifa lolote lile. Maana watu ndio wanaoleta maendeleo katika nchi., watu ndio wanaobuni vitu, watu ndio wanaolipa kodi, watu ndio wanaoleta mawazo mazurikwaajili ya maendeleo ya nchi yao n.k.
Pia idadi halisi ya watu ndiyo itakayotusaidia kuwa na uwakika wa kile tunachotaka kufanya katika taifa letu na katika taasisi yoyote ile. Pia idadi halisi ndiyo itakayotusaidia kusonga mbele pamoja na Mungu.
Ndugu watanzania wenzangu kundi lolote huanza kuhalibika,au kupotea unapoondoa macho yako kulitazama. Rais Samia Suluhu Hassan kufanya uwamuzi wa wananchi wake kuhesabiwa si uamuzi mdogo huo, anataka kujua tupo wangapi?Tupo wapi? Je mahitaji yetu ni nini? Wangapi wanauwezo wa kulipa kodi? Wangapi hawana uwezo wa kulipa kodi na kwa nini? Tuwe tayali kuhesabiwa alisema
Takwimu sahihi za makundi mbali mbali za makundi ya watu ni za msingi sana, maana ndio zinazoweza kuainisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalumu kama, walemavu, vikongwe, watoto, wazee, vijana n.k.
Sensa ya watu na makazi itachochea ukuaji wa maendeleo na kuanzisha maono mapya ya taifa n.k. hatuwezi kupanga mipango inayohitaji utekelezaji bila kujali idadi ya watu wake. Ndugu zaku mipango yoyote bila takwimu hukumu yake ni umaskini.
Askofu Emmanuel Mwakandulu alisisitiza jambo hili kwa kunukuu maandiko matakatifu kutoka katika Biblia HESABU 1:2-3, LUKA 2:1-5 alisema Mimi, kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba watanzania wenzangu kutoa ushilikiano kwa serikali ya mama yetu Samia Suluhu Hassan tuwe tayari kuhesabiwa tarehe 23/08/2022. Sensa ni swala la kisheria, sense ni kwa mujibu wa sheria ya Takwimu No.351. kukataa kuhesabiwa ni kukosea Serikali na watanzania wote. Basi kuwa tayari kuhesabiwa kwaajili ya maendeleo yako na watanzania wote. Mungu akubariki sana nipo tayari kuhesabiwa.
Askofu Emmanuel Mwakandulu wa kanisa la Baptist jimbo la Dodoma mjini
Related Posts:
MBUNGE DITOPILE TUNAKUSHUKURU RAIS KWA KUTUPATIA WAKULIMA MBOLEA YA RUZUKU Na. Kadala Komba Dodoma MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkulima, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya Kilimo ambapo kwa mara ya kwanza b… Read More
MCHUNGAJI CHARLES PROSPERITY KUHESABIWA HAKUNA MAHUSIANO NA MAMBO YA GIZA KISHETANIWA YA USHETANINa. Kadala Komba Dodoma MCHUNGAJI kiongozi Charles A. Prosperity wa kanisa la The Covenant Place lililopo kisasa Relini Dodoma amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ya watu na makazi ambalo linatal… Read More
ASKOFU DKT. MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU NA. MWANDISHI WETU. Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 … Read More
MATUKIO KATIKA PICHA ;BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WANASIASA WALIOHUDHURIA JUBILEI YA MIAKA 50 MATUKIO KATIKA PICHA: Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wanasiasa waliohudhuria adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya miaka 50 ya Jimbo Katoliki Singida pamoja na Miaka 25 ya Upadre wa Mhashamu Edward Elais Mapunda Askofu … Read More
WAKAZI WA GAIRO MKOANI MOROGORO WAVAMIA LORI LA MAFUTA #MOROGORO: Wakazi wa Gairo mkoani Morogoro wamevamia tena lori la mafuta lililopinduka ili kujipatia mafuta. - Majeraha ya ajali kama hiyo iliyotokea miaka miwili iliyopita nakuuwa zaidi ya watu 100 bado hayajapona na idadi … Read More
0 Comments:
Post a Comment