Home »
» CHANJO YA POLIO MZUNGUKO WA 3 KUTOLEWA NYUMBA KWA NYUMBA DODOMA
CHANJO YA POLIO MZUNGUKO WA 3 KUTOLEWA NYUMBA KWA NYUMBA DODOMA
Na.Kadala Komba Dodoma
Bi. Lotalias Gadau afisa mradi mpango wa Taifa wa chanjo wizara ya afya amesema lengo la semina hii kwa waandishi wa habari ni kuwakumbusha kuhusiana na kampeni ya chanjo ya matone ya polio ya awamu ya Tatu ambayo inatalajiwa kuanza kutolewa tarehe 1 hadi 4 Septemba mwezi hujao.
Hayo yamejili mkoani Dodoma wakati wa semina na waandishi wa habari Bi. Lotalias Gadau altoa Taharifa alisema hadi sasa nchi yetu hatuna kisa chochote cha mgonjwa wa polio tangu mwaka 1996 tulipopata kisa cha kwanza hadi sasa hivi hatuna kisa chochote kile ambacho kimeweza kujitokeza pamoja na kwamba nchi za jirani kama Malawi na Msumbiji wenzetu wamepata visa kadhaa vya watu ambao wamepata ugonjwa wa polio.
“Kwetu Tanzania kama nilivyosema awari hatuna kisa chochote cha polio lakini kwenye nchi ya Malawi wana wagonjwa wawili waliopatikana na Msumbiji wana wagonjwa wanne ambao wamepatikana tangu mlipuko wa polio ulivyotangazwa mwezi Februari 2022.
Aliongeza kuwa hawa ni majirani zetu na hata ukiangalia kwenye sayansi inavyosema kukitokea kisa kimoja eneo furani tutegemee kwamba kuna mamia ya watu wameathilika kwaiyo sisi na Msumbiji na Malawi kwakuwa ni majirani tunashilikiana maswala ya kibiashara hata ya kifamilia hata kuna familia wengine wameoa na kuolewa huko, kuna athari kubwa au kuna hatari kubwa kwamba sisi kama nchi tunaweza tukaipata endapo hatutajidhatiti, lakini naweza nikasema kwamba sisi kama nchi tumejidhatiti vya kutosha ndio maana tumefuata taratibu zote kwamba taratibu za kimataifa zinasema kwamba ukitokea mlipuko nchi ya jirani au nchi yako wewe mwenyewe hakikisha unafanya kampeni ya watoto chini ya umri wa miaka mitano, kwasababu hao ndio ambao wanahathilika Zaidi ili kuweza kujikinga na ugonjwa huu.
“mlipuko awamu ya kwanza tumeenda mikoa ile ambayo imezunguka Malawi mikoa kama Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe lakini kwa awamu ya pili tulienda nchi nzima tulichanja watoto wote na awamu ya tatu tutaenda pia nchi nzima nabado tutaenda awamu ya nne ili kujidhatiti kwamba endapo hicho kirusi kitakua kinazunguka kwasababu majirani zetu wamekipata kikute watoto wamekua imara na wana kinga thabiti wasiwezekupata madhara yoyote.
Bi.Lotalis Gadau alisema Endapo mtu hajapata chanjo ya polio madhara makubwa ni mawili uwenda atapata ulemavu wa kudumu labda mguu au miguu yote miwili itapooza gafla akawa hanauwezo hata wa kunyenyuka ndio maana zamani ulikuwa unaona watu wanatembelea magongo ndicho kitakachoweza kumpata.
“ Na athari ya pili ni kwamba kifo cha gafla na kama hajafanya uchunguzi hutajua nikwamba amekufa kwaajiri ya polio au sababu nyingine kwaiyo madhara ni makubwa uwenda upate kilema cha kudumu au upoteze maisha.
Bi. Lotalis Gadu akisema Imani potofu ambazo zinachangia watu ambao hawana uwelewa na umuhimu wa chanjo anazani labda mtoto akipata chanjo anaweza kukosa nguvu za kiume au kama ni binti baadae asiwezekuzaa ndizo hizo Imani ambazo sana tunakuwa tukikumbana nazo. Kwasababu mimi siwezi kupoteza kupeleka mtoto akapate chanjo na hizo chanjo wameleta wazungu kwanza zina vitu vya ziada ambavyo vitawafanya watoto wetu wasiweze kuzaa hapo baadae, hizo ndio Imani potofu ambayo imekua ikitawala maeneo mengi.
“Chanjo itatolewa kwenye nyumba za Ibada katika hili kwanza kabisa kabla hatujakaa na waandishi tulikaa na viongozi wa madhehebu ya dini wale viongozi wao wa juu kabisa tukawaomba wawaelekeze watu wao wamatawi yao chini kwamba kutakua na kampeni na isitoshe kila mkoa, kila wilaya pia wamefanya vikao na viongozi wao wa dini, kwaiyo viongozi wote wanajua na wameandikiwa barua, barua zimesomwa kwenye misikiti, nyumba za ibada kwamba tarehe 1 hadi 4 kutakua na kampeni kwaiyo waumini wanajua na tumewaomba maana kuna wengine wanakua ni ngumu kupatikana siku za kawaida kwaiyo siku ileile ya ibada wakimaliza watakutana na mchanjaji yupo mlangoni na chanjo zake anawasubili wakimaliza ili aweze kuwachanja .
Chanjo ni ileile inayotumika kwa njia za kawaida kwenye kampeni tunalenga kuwakusanya watu wengi Zaidi kwasababu kwenye kampeni haijalishi wewe mtoto wako alipata chanjo jana au juzi kwenye kampeni tunazoa wote chini ya miaka mitano.
Bi. Lotalias Gadau afisa mradi mpango wa Taifa wa chanjo wizara ya afya akitoa taarifa kwa waandishi wa habari umuhimu wa Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka mitano
Waandishi wa habari wakiendelea kufutilia taarifa ya chanjo ya Polio
Dr Bujite akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Related Posts:
MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AMETOA MAELEZO KUHUSU AJALI YA NDEGE*YALIYOJIRI LEO NOVEMBA 14, 2022 WAKATI MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI - MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AKITOA TAARIFA YA MAELEKEZO YA BARAZA LA MAWAZIRI KUHUSU AJALI YA NDEGE YA KAMPUNI YA PRECISION AIR IL… Read More
WAZIRI SIMBACHAWENE, AMPONGEZA MAMA TUNU PINDANa Mwandishi wetu Kuimba kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuewa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa. Kauli hiyo imetolewa na W… Read More
UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KULETA TIJA KWA WATANZANIANaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amebainisha kuwa, biashara ya Makaa ya Mawe inatarajia kuleta tija kwa Watanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo ndani na nje ya nchi. Dkt. Kiruswa ameeleza hayo Novemba… Read More
“MBEYA INAENDA KUFANANA NA HADHI YA MAJIJI, TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA” DKT. TULIA*Na. Mwandishi Wetu Mbeya Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi wa Mbeya Mjini kumshukuru na kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa… Read More
WALIMU WA SHULE BINAFSI NA SERIKALI WAMEUNGANA KWA PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO MASHULENINa. Kadala Komba Dodoma Mwenyekiti wa shule za awali za Binafsi Mkoa wa Dodoma Ester Manyanda Akizungumza na Waandishi wa Habari lengo la kukutana pamoja Walimu wa Shule Binafsi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Do… Read More
0 Comments:
Post a Comment