Subscribe Us

SIDO IMETOA MIKOPO YENYE THAMANI YA MILIONI 200 KWA WAJASIRIAMALI.

 
  
Na Sifa Lubasi,Dodoma 


MENEJA wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dodoma Twaha Swedi amesema wametoa mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa kipindi cha mwaka moja kwa wajasiriamali wadogo na wachakataji wa mazao ya kilimo.
Akizungumza jana wakati wa mahojiano kwenye  maonesho ya wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini hapa,a'lisema kuwa kati ya waliopata mikopo hiyo wamo wazalishaji wa mvinyo na mafuta ya alizeti.
"SIDO hutoa mikopo kwa wajasiamali wadogo na  wa kati (SME's) kwa ajili ya kukuza mitaji ya miradi mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye sekta za biashara,uzalishaji pamoja na uwekezaji kwenye miundombinu ya biashara,zana na vifaa vya uzalishaji,"alisema.
Alisema kuwa mwaka huu zaidi ya wakulima 100 wa zabibu na alizeti wamewezeshwa mikopo,  elimu na matumizi ya teknolojia rahisi za Kilimo na usindikaji.
"Wakulima wa zabibu, alizeti na mazao mengine ya kimkakati wamenufaika na fursa mbalimbali kwenye mikopo kupata masoko ya ndani na kimataifa,"alisema 
Alisema kuwa SIDO mkoa wa Dodoma imetoa mikopo yenye zaidi ya Sh milioni 200 katika maeneo tofauti kwa wachakataji na wafanyabiashara wadogo wadogo 
Pia alisema  katika kutekeleza dira ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050 Shirika hilo limejipanga katika kusaidia wakulima wa zao la zabibu na mazao mengine ya kimkakati kwenye matumizi ya teknolojia rahisi, kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi.
" Shirika  limejipanga kutekeleza dira ya 2025-2050 kwa kusaidia wakulima wa zabibu, alizeti na mazao mengine ya kimkakati kwenye mnyororo wa thamani,"alisema
Aidha alisema wakulima na wasindikaji wamekuwa waliopata elimu ya kutambua jinsi matumizi ya teknolojia rahisi zinavyoweza kusaidia katika kuchakata mazao ya kilimo.
Pia alisema wamejipanga kuwa na ofisi kila wilaya katika mkoa wa Dodoma na wameanza na wilaya ya Kondoa .
Alisema kuwa mikakati nyingine ni kuinua vikundi cikinsu iya vijana na kimamama kwani nguvu kubwa ya uzalishaji iko kwenye maeneo hayo.
Mwisho


 


0 Comments:

Post a Comment