Subscribe Us

EAGT IMEWATAKA WACHUNGAJI WANAOONDOKA KUACHA MALI ZA KANISA

Na. Kadala Komba Dodoma

Askofu Mkuu wa kanisa la The Avngelistic Assemblies of God Tanzania Dkt Brown Mwakipesile Amesema kumekuwa na migogoro mingi ndani ya kanisa letu kwa muda mrefu takriban miaka 6 uliotokana na aliyekuwa Makamu Askofu Mkuu wa kanisa letu  John Stephene Mahene kupinga kuondolewa madarakani kwa sababu za kukiuka miongozo ya imani ya kanisa hilo ambapo alidai kuondolewa kwa sababu za kuhoji ubadhilifu wa fedha na mali za kanisa uliofanywa na viongozi wa kanisa.

Hayo yamejili jijini Dodoma  wakati Askofu Dkt. Brown Mwakipesile akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za za kanisa Meriwa  Alisema Ndugu wanahabari tumewaita leo kueleza mustakabali mzima wa mgogoro huo ambapo kutokana na maamuzi ya uongozi wa Msajili wa Jumuiya ulitoa barua yenye kumbukumbu Na.SA. 7183/PARTVI/50 ya tarehe 30June, 2022, barua ambayo ina maelezo ya kina sana  jinsi Serikali ilivyofanya Uchunguzi wa kutosha na mwishowe ikabaini kwamba tuhuma zote walizotuhumiwa Viongozi Wakuu wa Kanisa la EAGT hazina msingi na wala Viongozi hao Wakuu hawahusiki kabisa na tuhuma zote walizotuhumiwa nazo, jambo ambalo limeipa ujasiri Serikali yetu kutangaza kwamba, mgogoro umekwisha na kutambua Viongozi   halali wa Kanisa la EAGT kwa sasa kwa kuorodhesha majina  yao  jambo ambalo limefuta kabisa mawazo potofu yaliyokuwa yanaenezwa  kwamba kuna EAGT mbili Alisema Askofu Mwakipesile.

Sambamba na hilo Askofu Mwakipesile ametambulisha majina halali ya viongozi wa kanisa hilo.
1.Askofu Mkuu Dkt. Brown Abel Mwakipesile
2.Makamu Askofu Mkuu Dkt. Joshua Benjamin Wawa
3. Katibu Mkuu Dkt. Leonard Majura Mwizarubi
4.Mhuzani Mkuu Dkt. Praygod Zawadi Mgonja
5.Mshauri Mkuu Dkt. Livingstone Dennes

Aidha Askofu Mwakipesile alisema kwa maamuzi haya ya Serikali, kikao cha Baraza la Waangalizi wa Kanisa letu zuri la EAGT kilichokaa tarehe 12/07/2022 ambacho ndicho kikao chenye kauli ya mwisho ya kukata mashauri mbalimbali kuhusiana na Wachungaji. Toleo la 2011 Ibara ya XI- 4 kifungu kidogo (f) kilimshukuru Mungu sana  pamoja na Serikali yetu kwa kutenda haki, na kisha kikatamka kwamba.

Sambamba na hilo Askofu Mwakipesile ametoa miezi mitatu kuanzia tarehe ya barua hii kwa Mchungaji yeyote atakayetaka kurejea baada ya mgogoro kumalizika, atapokelewa na ngazi husika kwa sharti la kuandika barua kwa Uongozi husika kwamba ametambua kosa lake na sasa anaomba msamaha na kwamba yuko tayari kutumika chini ya Uongozi halali wa Kanisa la EAGT. Mwisho wa kupokelewa ni tarehe 20 Octoba 2022; na baada ya tarehe  hiyo mlango utakuwa umefungwa Alisema .

Aidha Askofu Mwakipesile alisema kwa  wale ambao watataka kuondoka EAGT, Baraza la Waangalizi limetamka kwamba lazima waheshimu sana Katiba yetu ya EAGT Toleo la 2011 Ibara ya IX  ambayo inasema,”Mtumishi aachapo utumishi wake EAGT ataondoka pekee pasipo washirika wala mali za Kanisa”
Kanisa la EAGT litaendelea kudumisha amani ya nchi yetu kama ambavyo limekuwa likifanya siku zote.

Pia Askofu Mwakipesile alisema kwa Sasa Kanisa la EAGT  litaendelea kudumisha  amani na utulivu katika kutekeleza majukumu yake kwa busara pamoja na hekima itokayo juu kwa maongozi ya Roho Mtakatifu kwani ndiyo msingi wa kanisa letu, huku tukihubiri habari njema ya watu kuacha dhambi na kumgeukia Kristo kusimamia utakatifu kwa bidii,  Mungu awabariki. Yak. 3:17-18

Mwisho kabisa Askofu Mwakipesile alisema nitumie fursa hii pia kuwasihi watanzania wote kushiriki katika zoezi la Sense ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022 ikiwa ni zoezi muhimu kwa kila mmoja wetu kuhesabiwa ambapo tunaamini itaisaidia Serikali kuendelea kuweka mipango mbalimbali ya kimaendeelo kwa kujua idadi ya watu wake.
 
                                                MWISHO

 

0 Comments:

Post a Comment