Home »
» IDARA YA MAAFA YAWAPIGA MSASA WABUNGE
IDARA YA MAAFA YAWAPIGA MSASA WABUNGE
Na. Mwandishi wetu.
Idara ya Menenjimenti ya Maafa imefanya semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimaizi wa Maafa ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu sheria na namna zinavyofanya kazi pindi maafa yanapojitokeza.
Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma ikihusisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Idara ya Menejimenti ya Maafa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa jukumu la kuratibu na kushughulikia maafa na dharura zote ikijumuisha shughuli za Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali.
Viilevile Shughuli za kila siku za Idara zinaongozwa na Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na sheria ya Menejimenti ya Maafa Na.7 ya mwaka 2015.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa Semina ya kuijengea uwezo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Agosti 31, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Charles Msangi akiwasilisha mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka (kulia) akichangia hoja wakati wa semina hiyo na (kushoto) ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Ngw’asi Kamani.
Sehemu ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia semina hiyo katika Ukumbi wa Bunge Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati semina hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
0 Comments:
Post a Comment