Subscribe Us

HUDUMA ZA UGANI KUPITIA MATUMIZI YA TEHAMA IMEIMARISHWA VYEMA.

 
Na Sifa Lubasi,Dodoma


MRATIBU wa Programu ya Uhimilivu wa  Mifumo ya Chakula  Nchini, Timoth Semuguluka amesema kuwa wameimarisha huduma za ugani kupitia matumizi ya Tehama ili wakulima waitumie  kupata huduma za ugani pale walipo
.Alisema hayo jana Jijini hapa kwenye maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni,
Mratibu huyo alisema kuwa wameimarisha mifumo ya kidigitali iliyopo na kutengeneza mifumo rafiki ili wakulima waitumie ili kupata huduma za ugani
Alisema kuwa program ya ugani inalenga kuimarisha upatikanaji huduma ya ugani kwa mazao ya chakula na biashara,kwani ni daraja kati ya teknolojia kwenda vituo vya utafiti Kisha kwaa wakulima.
Alibainisha kuwa mahitaji ya maofisa ugani ni 20,000 lakini waliopo ni 7,000 tu, mapungufu yaliyopo ni zaidi ya asilimia 50“ a'lisema
"Tunachokifanya ni kutumia mifumo ya kidigitali iliyopo na kutengeneza mifumo rafiki ili wakulima waitumie ili kupata huduma za ugani, maofisa ugani wamesajiliwa kupitia mifumo hiyo kupitia simu zao na wamekuwa wakiulizwa maswali na wakulima wamekuwa wakipata masuluhisho mbalimbali,” alisema
Alitaja maeneo mengine ya utekelezaji ni pamoja na kufanya utafiti wa teknoloijia mbalimbali za mbegu za kilimo zinazohimili mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha mifumo ya upatikanaji na udhibiti wa mbegu bora, kuimarisha usimamizi na utumiaji wa miundombinu ya umwagiliaji, kuandaa mfumo mpya wa usimamizi wa uendeshaji wa ghala zote za umma, kupima afya ya udongo katika vijiji vyote vya Tanzania bara  na kuandaa ramani ya afya ya udongo.
Pia alisema lengo la program hiyo ni kuongeza ufanisi, kuleta matokeo chanya ya uwekezaji wa raslimali za umma na masuala ya kisera
,“Utekelezaji wa program hii utaongeza tija na mchango wa uwekezaji wa serikali unaolenga kupunguza athari zinazotokana na uhaba wa maji kwenye mifumo ya mwagiliaji iliyopo na kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna,” alisema
Alisema kuwa program hiyo inatekeleza vipaumbele vya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo, sehemu ya mazao ikiwemo ununuzi wa vifaa vya kupimia udongo, ujenzi wa nyumba za maofisa ugani, ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa maabara ya kudhibiti wa ubora wa mbegu, uchimbaji wa visima kwa ajili ya umwagiliaji, ujenzi wa maabara ya tissure culture,Pia uzalishaji wa mbegu, ukarabati wa vituo vya maonesho ya nane nane.
mwisho


 


0 Comments:

Post a Comment