Na.Kadala Komba Dodoma
Askofu wa
kanisa la International Evangelism Church Mkoa wa Dodoma Silvester
Thadey amesimulia alivyokuwa mlevi na maisha yalivyompiga kabla ya
kuokoka.
Askofu Thadey
amesema ameona awasimulie washirika wake kuhusu maisha yake ya nyuma
kabla ya Wokovu maisha ambayo aliishi,kwani alikuwa mlevi Hali
iliyopelekea maisha kuemchanganya na kutoona mbele nakujaribu kuenda
mikoa mbalimbali kutafuta maisha lakini bado mambo yakawa magumu kwa
upande wake na Rafiki yake.
Hayo
yamejili jumapili ya tarehe 14/8/2022 jijini Dodoma katika Ibada ya
kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kumaliza salama Mfungo wa maombi ya wa
wiki moja ya kuombea Amani ya Nchi wakati akihubiri injili ambayo
ilibeba ujumbe unaosema USIKATE TAMAA KWA MUNGU LIPO TUMAINI.
Aidha
alinukuu vifungu mbalimbali katika Biblia kikiwepo kifungu Cha Isaya
4:5.6 ambapo amesema pamoja na kuwa na maisha mabaya ambayo
hayakumpendeza Mungu siku moja alisikia habari njema za Mungu ndipo
akaamua kutoa maisha yake kwa kumpokea Yesu ndipo ukazaliwa na wito wa
Utumishi.
"Wakati
mwingine Mungu anakuwa na mipango nikubwa kwajili ya maisha yetu lakini
kwa sababu atujafanya maamuzi, lakini pindi unapofanya Maamuzi Basi
Mungu anaamua kukuita ili uweze kumtumikia kwa kusudi maalumu.",amesema
Sambamba
na hilo Askofu Thadey Aliwataka Wakristo kuacha tabia ya kukimbilia
miujiza na badala yake wajikite katika kuliamini Neno, sababu ukiliamini
Neno ndani ya Neno uko muujiza wa kweli, Yesu alitabiri siku za mwisho
mtaona ishara nyingi na mambo ya ajabu yakitokea, hivyo kitu kikubwa ni
kuyakabidhi maisha kwa kristo Yesu baadaye utaona miujiza.
Katika
hatua nyingine Askofu Thadey alitumia nafasi hiyo kuwaeleza Waumini wa
kanisa hilo umuhimu wa kushiriki katika uandikishaji wa sensa ya watu na
makazi itakayo fanyika Agost 23 Mwaka huu Nchini.
Askofu Silvester
Thadey wa
kanisa la International Evangelism Church Akiwaombea Baraka washirika wa kanisa hilo |
Waumini wa kanisa la Internation Evangelism Sinai Ipagala Dodoma wakimsikiliza kwa makini Askofu wa Kanisa hilo |
- MWISHO
0 Comments:
Post a Comment