Home »
» WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA ARDHI WA MIAKA MITATU KINONDONI
WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA ARDHI WA MIAKA MITATU KINONDONI
Na. Mwandishi wetu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mitatu katika eneo la Boko-Dovya, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam baina ya Bw. Aloyce Mwasuka na Bw. Salutari Massawe.
Katika mgogoro huo unaohusisha viwanja namba 393, 395 na 370 kwenye kitalu G (Boko Dovya) vilivyoko njia panda ya Mbweni, Bw. Massawe alijenga ukuta ambao ulikuwa unazuia matumizi ya barabara na hivyo kumfanya Bw. Mwasuka apitie kwa jirani yake Bi. Oliver Semuguruka (kiwanja na. 395) ili aweze kufika nyumbani kwake (kiwanja na. 393).
Akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, watendaji wa Wilaya ya Kinondoni katika kikao alichokiitisha leo (Jumatano, Agosti 17, 2022) ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na hatua aliyoichukua Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Godwin Gondwe ya kusimamia uvunjaji wa ukuta huo ili kupisha eneo la barabara.
“Ninakushukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na timu yako kwa kuchukua hatua tangu jana ili kusimamia haki ya wananchi wasio na uwezo. Haki ni ya kila mmoja, mwenye uwezo na asiye na uwezo. Ile barabara iboreshwe ili wananchi wote wanufaike,” amesema.
Waziri Mkuu amesema hatua hiyo inaenda sambamba na utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyowapa wasaidizi wake akitaka wahakikishe kuwa wananchi hawapati shida kwenye maeneo yao.
Akisisitiza usimamizi wa majukumu yao kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri Mkuu amesema: “Nendeni mkasimamie masuala ya ardhi ili Watendaji wa Serikali nao wafanye kazi nyingine za kuwahudumia wananchi. Lazima tufanye mifumo isimamiwe ili kazi nyingine ziendelee,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Ridhiwan Kikwete alisema Wizara itaendelea kusimamia migogoro yote iliyopo na kuweka mpango wa kuishughulikia.
Related Posts:
TAGAZO LA NAFASI ZA KAZI MTENDAJI WA KIKIJI,MADEREVA, MSAIDIZI MTUNZA KUMBUKUMBU WANAHITAJIKA … Read More
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI … Read More
MATUKIO YA PICHA ZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA DODOMA Na. Kadala Komba Dodoma Maonesho ya Nanenane kitaifa yamefunguliwa rasmi tarehe 1,Agosti, 2024 Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa hadi Agosti 8,2024 ambapo Elimu m… Read More
MBUNGE NOLLO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MIRADI MINGI YA MAENDELEO JIMBO LA BAHI Na. Kadala Komba Bahi Haya yamebainishwa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo wa Bahi Kenneth Nollo katika mkutano wa hadhara aliyofanya Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyemule akisikiliza kero za wananchi kata ya Ba… Read More
*INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UBORESHAJI KUTUNZA VIFAA* Na Mwandishi wetu, KigomaTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetaka watendaji wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Kigoma kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vikaweze kutumika m… Read More
0 Comments:
Post a Comment