Home »
» WFP YAKABIDHI VIFAA VYA MAWASILIANO KWA OFISI YA WAZIRI MKUU
WFP YAKABIDHI VIFAA VYA MAWASILIANO KWA OFISI YA WAZIRI MKUU
Na Mwandishi wetu-Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga amepokea vifaa vya mawasiliano vitakavyotumika katika kukabiliana na maafa mbalimbali hapa nchini ambavyo ni Ndege zisizo na Rubani (Drones) vyenye thamani ya shilingi Milioni 102,741,400 vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma Mhe. Ummy alisema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu kutekeleza shughuli za uratibu na udhibiti wa maafa mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa katika picha ili kupata majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.
Mhe. Ummy alieleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.
“Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”Alisema Mhe. Ummy.
Aidha aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu alibainisha kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.
“Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukuwa mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa uraisi”.
Aidha Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gibson alifafanua kuwa mradi huo ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na viupembeel vya serikali na kuwekeza katika kilimo, elimu, maafa pamoja na wakimbizi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza kabla ya kupokea vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya mikutano kwa njia ya mtandao katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (kushoto) akipokea Kompyuta mpakato kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gibson (kulia) ikiwa ni ishara ya kupokea vifaa hivyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akifafanua jambo wakati wa Makabidhiano ya vifaa hivyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Related Posts:
ANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUUWA NCHI WANACHAMA Na Mwandishi wetu- Dodoma Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Ji… Read More
WOWAP WATOA FEDHA TASLIMU KWA WANAFUNZI IKIWA NI MWENDELEZO WA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE … Read More
RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI WA KATIBU MKUU … Read More
CHUO KIKUU CHA UDOM KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA COLONYNa Sifa Lubasi, Dodoma CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Colony kilichopo Ujerumani kimefanya warsha ya watafiti wa kuhifadhi maarifa asilia kwa kuwashirikisha wataalam kutoka nchi tisa dunian… Read More
WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA NAIBU WAZIRI MKUU CHANGAMOTO YA MAFUTA Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko aendelee kushughulikia suala la changamoto ya upatikanaji wa nishati ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini.“...Wata… Read More
0 Comments:
Post a Comment