Home »
» MBUNGE DITOPILE TUNAKUSHUKURU RAIS KWA KUTUPATIA WAKULIMA MBOLEA YA RUZUKU
MBUNGE DITOPILE TUNAKUSHUKURU RAIS KWA KUTUPATIA WAKULIMA MBOLEA YA RUZUKU
Na. Kadala Komba Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkulima, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya Kilimo ambapo kwa mara ya kwanza bajeti ya Uzalishaji wa Mbegu imeongezeka kutoka Sh Bilioni 10.5 hadi Sh Bilioni 43.03.
Hayo ameyasema jijini Dodoma katika mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesema kwa kipindi kifupi cha Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan mageuzi makubwa yamefanyika katika sekta ya Kilimo kulinganisha na miaka ya nyuma ambapo kilio kikubwa kilikuepo.
Amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi amewezesha kupatikana kwa bajeti bora ya Kilimo ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 Wizara ya Kilimo imetengewa Sh Bilioni 751 huku Sh Bilioni 631 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Mbunge Ditopile ameongeza kuwa ongezeko la Bajeti ya Kilimo kwa mwaka huu wa fedha ni takribani asilimia 300 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2020/21 ambapo kiasi kilichotengwa ni Sh Bilioni 229 na kati ya fedha hizo ni Sh Bilioni 150 pekee ndio zilienda kwenye miradi ya maendeleo.
” Rais Samia pia amejidhatiti kwenye eneo la tafiti za Kilimo, Bajeti ya tafiti za Kilimo imepanda kutoka Sh Bilioni 7.3 kwa mwaka 2020/21 hadi Sh Bilioni 40 kwa mwaka huu wa fedha. Tunamshukuru Rais pia kwa kupandisha bajeti ya Uzalishaji mbegu kutoka Sh Bilioni 5.4 hadi Sh Bilioni 43 kwa mwaka huu wa fedha 2022/23.
Pia tumeshuhudia utaratibu mzuri wa kuwawezesha wakulima nchini kupata Mbegu za Alizeti ambapo gharama zote ni Sh 3,500 tofauti na bei ambayo haikua na ruzuku ambayo ilikua ni kSh 7,000 hadi 8,000,” Amesema Mbunge Ditopile.
Amesema kwa namna ambavyo Rais Samia ameonesha mageuzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo wao kama Wakulima.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile akizungumza na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mh. Mariam Ditopile
Related Posts:
HUAWEI AT MWC SHANGHAI 2023:BOOSTING 5G EVOLUTION TOWARDS 5.5G REVITALIZE THE DIGITAL ECONOMYHuawei has shown up in full force for MWC Shanghai 2023, with their activities all falling under their theme of "GUIDE to the Intelligent World". This year, the company's activities include an experiential tour that takes aud… Read More
WAPIGA KURA 74,642 KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO Na Mwandishi maalum - NECWapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.Jumla ya w… Read More
*MASHINE YA MRI IMEANZA KUFANYA KAZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA*Na Mwandishi wetu Mbeya.Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe Julai 12, 2023 imeanza rasmi kutoa huduma ya vipimo kwa kutumia mashine ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa MRI (Magnetic Resonace Imaging)Akiongea baada ya … Read More
SERIKALI HAIPO TAYARI KUMPOTEZA MTU Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Serikali haipo tayari kuona Mwananchi yeyote anapoteza uhai wake kwa sababu za ama ujambazi au udereva mbovu barabarani au migogoro ba… Read More
WANANCHI WAALIKWA MIAKA 60 YA JKT Na Moreen Rojas,Dodoma.Waziri wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)Mhe.Innocent Bashungwa amewaalika wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yatakayofanyika tarehe 10 julai siku ya jumatatu … Read More
0 Comments:
Post a Comment