Subscribe Us

WAKULIMA WA ALIZETI KANDA YA KATI KUNUFAIKA NA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MAINLAND

 
Na Sifa Lubasi,Dodoma


MKUU wa Wilaya ya Singida Mjini, Godwin Gondwe amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na kiwanda cha mafuta ya alizeti cha kampuni ya Mainland utaleta uhakika wa masoko ya alizeti ya wakulima wa mikoa ya Singida na Dodoma.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kwenye maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma,Gondwe alisema kuwa  ujio wa kiwanda hicho Ni suluhisho la mazao ya wakulima wa alizeti.
"Hili litakuwa suluhisho kubwa la soko la wakulima wa kanda ya kati, kwani watakuwa na soko la uhakika"alisema 
Kwa upande wake Ofisa mauzo wa kiwanda hicho, Castro William alisema kuwa kiwanda hicho kipo eneo la Veyula jijini Dodoma ambapo uwekezaji huo kufikia takribani dola milioni 30 unaochukua eneo la mita za mraba 162,000.
A'lisema kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho cha kuzalisha mafuta ya alizeti Dodoma kutasaidia ukuaji wa kampuni katika bara la Afrika na kuchangia uzalishaji na biashara ya bidhaa za mazao ya kilimo Afrika Mashariki.
Alisema uwekezaji huo mkubwa unalenga kuzalisha mafuta safi ya kupikia,salama na yenye afya.
"Kampuni  itazalisha aina mbili za mafuta iliwemo Merrin Farm ambapo mafuta hayo yamesafishwa na yenye ubora wa hali ya juu ,hutengenezwa kwa mbegu za alizeti safi kwa asilimia 100,"alisema 
Alisema kuwa aina nyingine ni Sunland ambayo ni mafuta ya alizeti yaliyosafishwa hutengenezwa kwa mbegu za alizeti safi, asili  kwa asilimia 100 yenye wingi wa mafuta yatokanayo na mimea na vitamin E yanasaidia lishe bora,kwa afya ya moyo.
Mwisho


 


0 Comments:

Post a Comment