Na.Kadala Komba Dodoma
SHIRIKA la Foundation for Civil Society FCS AZAKI
limetoa ruzuku yenye jumla ya Shilingi bilioni nne kwa Asasi za kiraia
AZAKI 89Tanzania bara na Visiwani ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo
chini ya program za utawala bora katika sekta za maji,elimu afya na
kilimo ikiwemo usawa wa kijinsia kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo,Francis Kiwanga ameyaeleza hayo leo Jijini
Dodoma wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa ruzuku kwa Asasi hizo
zilizochaguliwa baada ya kukidhi vigezo ambapo miradi hiyo imejikita ili
kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi kuboresha maisha
yao na kukuza Sekta ya Asasi za Kiraia.
Aidha
amesema kuwa Shirika hilo limepitisha mpango mkakati mpya wa Mwaka 2022
hadi2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa,wanawajibika na
wanapata haki za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha
yao.
Benadeta
Choma wa Asasi isiyo ya kiraia ya Tanzania women initiative iliyopo
Mkoani Tanga amesema kuwa Kama NGOS kwa ruzuku walizopata zitawasaidia
kujenga uelewa kwa wananchi katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS,Francis Akizungumza na wajumbe kuhusu mpango mkakati mpya wa Mwaka 2022 hadi2026 |
0 Comments:
Post a Comment