Home »
» CHAMWINO YAJIWEKEA MPANGO MKAKATI WA KUONDOA ZIRO MASHULENI
CHAMWINO YAJIWEKEA MPANGO MKAKATI WA KUONDOA ZIRO MASHULENI
Na Peter Mkwavila CHAMWINO.
MKUU wa wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Gift Msuya amesema kuwa ili kuepukana na ziro shule za masingi na sekondari wamejiwekea mpango mkakati wa kuwasaka watoto wasioenda shule na ikiwemo na kwenye kaya zao wanaziishi kabla hawajadiliwa na uongozi husika wa kata na kijiji.
Alisema mpango huo wa kuondoa ziro katika wilaya hiyo umeanzishwa kwa kuwagawia misaada ya vifaa mbalimbali vya elimu zikiwemo shule nane za msingi na sekondari zilizopo kata ya Buigiri.
Ametaja vifaa hivyo vya elimu ni pamoja na kompyuta mashine ya kutoa cop vyenye thamani ya million 7.6 ili zitatumika kwa ajili ya kuepukana na ziro hizo mashuleni.
Msuya akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo kwenye uzinduzi wa Kanzi Data maalumu ya kwa ajili ya kumbukumbu ya kazi za walimu na wanafunzi uliofanyika Buigiri shule ya msingi ya Wasioona ya Buigiri Misheni,
Alisema kuwa hatua kwa kuanza imeanza kwa kata ya Buigiri ambayo imenunua vifaa hivyo ikiwa ni sehemu mojawapo mihimu ya kuunga juhudi kwa serikali ambayo moja wapo imewekewa mkazo ni elimu.
Alisema mkakati huo wa kuondoa ziro mashuleni pia haupo kwa upande wa serikali peke yake, bali pia kwa wadau wote wa elimu wakiwemo wazazi ,huku lengo likiwa kuwafanya watoto waweze kuwa na elimu iliyoboreshwa kwa kupitia vifaa vitakavyowawezesha kufanya vizuri kimasomo.
Hata hivyo msaada huo uliotolewa utawawezesha kusaidia wazazi katika kuondokana na umasikini kwa kupitia watoto wao ,endepo watakuwa karibu nao kwa kuwasomeshwa na kuwasimamia kielimu .
“Suala la elimu linaweza kuwa na mabadiliko ya maendeleo kwa kuwa watoto hao wakisomeshwa na kusimamiwa taifa linaweza kuwapata viongozi bora,wasomi,wataalamu mbalimbali ,madaktali walimu na wanasiasa”alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwiino Diwani wa kata ya Buigiri Keneth Yindi alisema kuwa kwenye kata yake wamejipanga kuboresha mazingira ya elimu na kwa kuanzia wamekabidhi shule hizo nane vifaa hivyo vya elimu.
Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kwenye kata hiyo ya Buigiri hakuna mwanafunzi yoyote ambaye hatojua kusoma na kuandika kutokana na kupatiwa kwa vifaa hivyo ambavyo vitatumika badala ya utaratibu uliopo wa hivi sasa.
Alisema ni imani kubwa kuwa elimu itakayopatikana kwa wanafunzi hao kwa kupitia vifaa hivyo itabadilisha taaluma na kuweza kufanya vema kitaaluma kwa kushirikiana na serikali,wadau wa elimu na wazazi.
Mwenyekiti huyo alizitaja shule zilizokabidhiwa ni pamoja na shule ya msingi Buigiri Blind,Uguzi,Mizengo Pinda,Chinangali Makibriut,Epypn na Buigiri Sekondari.
Mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya akizungumza na wakazi wa Kata ya Buigiri kwenye uzinduzi wa kanzi data maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya kazi za walimu na wanafunzi uliofanyika Buigiri Blind jana kushoto wa pili Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino
Keneth Yindi
0 Comments:
Post a Comment