Home »
» WATENDAJI WA SENSA WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
WATENDAJI WA SENSA WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Na mwandishi wetu
Watendaji wa Sensa wapewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 August 2022, wito huo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene.
“baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuna kazi kubwa ya Mchakato lazima tuwe tayari kusimama pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili zoezi liweze kukamilika”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es saalam.
Waziri Simbachawene ameipongeza kamati ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kufanikisha maamuzi ya kamati kuu ya Taifa ya Sensa.
“Vilevile napongeza Wizara zote, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi kwa ushirikiano mkubwa walioonesha wakati wote wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi”
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa amesema kwa wakuu wa kaya ambao hawatakuwa nyumbani wameandaa fomu maalumu ambayo itakuwa na maswali 11 ambayo itasambazwa kwa wakuu wote wa kaya kupitia kwa makarani wao wa sensa.
“Wakuu wa kaya waandike taarifa za watu ambao watakuwa wamelala usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kumrahisishia karani kujaza taarifa kwenye kishikwambi atakapofika kuchukua taarifa”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere convection Centre, Dar es saalam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es salam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza jambo kabla ya kikao na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Prof.Riziki Shemdoe kabla ya kikao.
Related Posts:
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 23, 2022… Read More
ASKOFU MWAKANDULU MIPANGO YOYOTE BILA TAKWIMU HUKUMU YAKE NI UMASIKINI Na. Kadala Komba Dodoma. Askofu Emmanuel Mwakandulu wa kanisa la Baptist jimbo la Dodoma mjini amesema Sensa sio jambo la kisiasa hili kujua idadi ya watu unaowaongoza lazima ujue idadi halisi ya watu, bali ni jambo la k… Read More
Waziri Simbachawene amshukuru Rais kwa fedha ya miradi maendeleoNa.Mwandishi Wetu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha billioni 16 kwa mwaka ulio… Read More
HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 24,2022 … Read More
WOSIA WA MAMA. BINTI YANGU YAJUE HAYA) NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI Mwanangu nisikufiche, watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari zao. Ukoo wa Mume na ukoo wa mke nao wanaoneshana umwamba hawa kwenye Send-off na hawa wanajibu kwenye harusi. Na ule usiku … Read More
0 Comments:
Post a Comment