Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

*NAIBU WAZIRI DKT. KIRUSWA AIHAKIKISHIA NCHI YA KOREA KUSINI FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI*

Na. Mwandishi wetu Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameihakikishia Nchi ya Korea Kusini kuhusu uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji katika Sekta ya Madini. Dkt. Kiruswa ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa kitaalamu wa African Minerals Geosciences Initiative (AMGI) uliolenga kuonesha maeneo ya kipaumbele sambamba na mkakati wa Serikali kuboresha taarifa za Jiosayansi uliofanyika Agosti 30, 2022 Jijini Dar es salaam. Alisema, mkutano huo umelenga kufunga awamu ya kwanza ya utafiti wa Jiosayansi uliofanyika katika nchi tatu zinazopakana ambazo ni Tanzania, Zambia na Msumbiji kati ya mwaka 2016 – 2021. Dkt. Kiruswa amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itahakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha kwa kuweka mazingira mazuri ya kushirikiana kufanya utafiti zaidi. Aidha, amewaeleza wawekezaji kuwa anatambua nchi ya Korea Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kiteknolojia duniani hatua inayopelekea kuwa na uhitaji mkubwa wa madini ya teknolojia kama vile kinywe, nikeli, niobium na REE. Naye, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Madini, aliishukuru Serikali ya Korea Kusini pamoja na Umoja wa Mataifa ya Afrika kwa kuamua kufanya mkutano huo nchini Tanzania na kuahidi kushirikiana katika kuangalia namna ya kufanya tafiti zaidi kwenye maeneo ya nchi. Kwa upande wake, Kamishna wa Madini Tanzania Dkt. Abdulraham Mwanga akizungumza wakati wa kuahirisha mkutano huo wa siku mbili kwa siku ya kwanza, aliwashukuru washiriki wote na kuwakumbusha kuwa madini ni kila kitu kwenye maisha ya sasa hivyo, ni vyema kama Bara la Afrika kukiwa na mkakati madhubuti wa kutambua rasimali madini na kuziendeleza. Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anatarajia kuwasilisha mada namna Benki hiyo inavyoweza kusaidia shughuli za jiosayansi kwa nchi za Afrika. Utafiti wa Jiosayansi ulifanyika katika maeneo ya Tunduma Mkoani Songwe na sehemu ya Wilaya za Tunduru, Namtumbo na Songea katika Mkoa wa Ruvuma chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika na kudhaminiwa na Serikali ya Korea Kusini. Mkutano huo umehudhuliwa na washiriki wa mradi wa AMGI kutoka nchi jirani za Zambia na Msumbiji, wawakilishi kutoka GST, wawakilishi kutoka Wizara ya Nyumba, Ardhi na Makazi Nchini Tanzania, Idara ya Upimaji na Ramani, ujumbe kutoka Idara mbalimbali za nchini Korea Kusini ambazo ni Consultancy; Mkurugenzi Msaidizi ofisi ya Kamishina wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi kutoka kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC).

IDARA YA MAAFA YAWAPIGA MSASA WABUNGE

Na. Mwandishi wetu. Idara ya Menenjimenti ya Maafa imefanya semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimaizi wa Maafa ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu sheria na namna zinavyofanya kazi pindi maafa yanapojitokeza. Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma ikihusisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Idara ya Menejimenti ya Maafa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa jukumu la kuratibu na kushughulikia maafa na dharura zote ikijumuisha shughuli za Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali. Viilevile Shughuli za kila siku za Idara zinaongozwa na Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na sheria ya Menejimenti ya Maafa Na.7 ya mwaka 2015.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa Semina ya kuijengea uwezo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Agosti 31, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Charles Msangi akiwasilisha mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka (kulia) akichangia hoja wakati wa semina hiyo na (kushoto) ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Ngw’asi Kamani.
Sehemu ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia semina hiyo katika Ukumbi wa Bunge Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati semina hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MTAKWIMU MKUU ASILIMIA 99.93 WAMEHESABIWA NCHI NZIMA

Na. Kadala Komba Dodoma MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema tangu kuanza kwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 Mwaka huu Nchini kote hadi kufikia Leo kiwango Cha Kaya zilizohesabiwa imefikia asilimia 99.93na zimebaki asilimia 0.07 tutaendelea kuhesabu Hadi tarehe 5 Septemba 2022. "Ambapo simu zilizotolewa zitatumika kuwafikia ambao hawajahesabiwa kwa kuwa utaratibu maalumu ulishaandaliwa wa namna ya kuzifikia Kaya hizo kupitia viongozi wa mitaa na vitongoji. Dk Chuwa ameyaeleza hayo Leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na zoezi hilo ambalo linamalizika rasmi kesho. Katika hatua nyingine amesema kuwa Sensa ya Majengo Hadi leo asubuhi tarehe 31Agosti, 2022 jumla ya majengo yaliyokwisha hesabiwa ni 6,351,927 Ambapo taarifa za umiliki,mahali yalipo na taarifa nyingine zinazoanisha katika Dodoso la majengo zimekusanywa.kwa makadirio ni kufikia Majengo Milioni 12. Aidha Dk.Chuwa amesema kama mnavyofahamu ,Sensa kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 imefanyika Sensa ya watu na makazi (Traditional Census) ya kidigitali ambayo imejumuisha Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi katika mfumo wake wa utekelezaji . "Alisema Ubunifu huu umeongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama ya kufanya mazoezi makubwa matatu ya kitaifa endapo yangefanyika katika kipindi tofauti.
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari

CHANJO YA POLIO MZUNGUKO WA 3 KUTOLEWA NYUMBA KWA NYUMBA DODOMA

Na.Kadala Komba Dodoma Bi. Lotalias Gadau afisa mradi mpango wa Taifa wa chanjo wizara ya afya amesema lengo la semina hii kwa waandishi wa habari ni kuwakumbusha kuhusiana na kampeni ya chanjo ya matone ya polio ya awamu ya Tatu ambayo inatalajiwa kuanza kutolewa tarehe 1 hadi 4 Septemba mwezi hujao. Hayo yamejili mkoani Dodoma wakati wa semina na waandishi wa habari Bi. Lotalias Gadau altoa Taharifa alisema hadi sasa nchi yetu hatuna kisa chochote cha mgonjwa wa polio tangu mwaka 1996 tulipopata kisa cha kwanza hadi sasa hivi hatuna kisa chochote kile ambacho kimeweza kujitokeza pamoja na kwamba nchi za jirani kama Malawi na Msumbiji wenzetu wamepata visa kadhaa vya watu ambao wamepata ugonjwa wa polio. “Kwetu Tanzania kama nilivyosema awari hatuna kisa chochote cha polio lakini kwenye nchi ya Malawi wana wagonjwa wawili waliopatikana na Msumbiji wana wagonjwa wanne ambao wamepatikana tangu mlipuko wa polio ulivyotangazwa mwezi Februari 2022. Aliongeza kuwa hawa ni majirani zetu na hata ukiangalia kwenye sayansi inavyosema kukitokea kisa kimoja eneo furani tutegemee kwamba kuna mamia ya watu wameathilika kwaiyo sisi na Msumbiji na Malawi kwakuwa ni majirani tunashilikiana maswala ya kibiashara hata ya kifamilia hata kuna familia wengine wameoa na kuolewa huko, kuna athari kubwa au kuna hatari kubwa kwamba sisi kama nchi tunaweza tukaipata endapo hatutajidhatiti, lakini naweza nikasema kwamba sisi kama nchi tumejidhatiti vya kutosha ndio maana tumefuata taratibu zote kwamba taratibu za kimataifa zinasema kwamba ukitokea mlipuko nchi ya jirani au nchi yako wewe mwenyewe hakikisha unafanya kampeni ya watoto chini ya umri wa miaka mitano, kwasababu hao ndio ambao wanahathilika Zaidi ili kuweza kujikinga na ugonjwa huu. “mlipuko awamu ya kwanza tumeenda mikoa ile ambayo imezunguka Malawi mikoa kama Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe lakini kwa awamu ya pili tulienda nchi nzima tulichanja watoto wote na awamu ya tatu tutaenda pia nchi nzima nabado tutaenda awamu ya nne ili kujidhatiti kwamba endapo hicho kirusi kitakua kinazunguka kwasababu majirani zetu wamekipata kikute watoto wamekua imara na wana kinga thabiti wasiwezekupata madhara yoyote. Bi.Lotalis Gadau alisema Endapo mtu hajapata chanjo ya polio madhara makubwa ni mawili uwenda atapata ulemavu wa kudumu labda mguu au miguu yote miwili itapooza gafla akawa hanauwezo hata wa kunyenyuka ndio maana zamani ulikuwa unaona watu wanatembelea magongo ndicho kitakachoweza kumpata. “ Na athari ya pili ni kwamba kifo cha gafla na kama hajafanya uchunguzi hutajua nikwamba amekufa kwaajiri ya polio au sababu nyingine kwaiyo madhara ni makubwa uwenda upate kilema cha kudumu au upoteze maisha. Bi. Lotalis Gadu akisema Imani potofu ambazo zinachangia watu ambao hawana uwelewa na umuhimu wa chanjo anazani labda mtoto akipata chanjo anaweza kukosa nguvu za kiume au kama ni binti baadae asiwezekuzaa ndizo hizo Imani ambazo sana tunakuwa tukikumbana nazo. Kwasababu mimi siwezi kupoteza kupeleka mtoto akapate chanjo na hizo chanjo wameleta wazungu kwanza zina vitu vya ziada ambavyo vitawafanya watoto wetu wasiweze kuzaa hapo baadae, hizo ndio Imani potofu ambayo imekua ikitawala maeneo mengi. “Chanjo itatolewa kwenye nyumba za Ibada katika hili kwanza kabisa kabla hatujakaa na waandishi tulikaa na viongozi wa madhehebu ya dini wale viongozi wao wa juu kabisa tukawaomba wawaelekeze watu wao wamatawi yao chini kwamba kutakua na kampeni na isitoshe kila mkoa, kila wilaya pia wamefanya vikao na viongozi wao wa dini, kwaiyo viongozi wote wanajua na wameandikiwa barua, barua zimesomwa kwenye misikiti, nyumba za ibada kwamba tarehe 1 hadi 4 kutakua na kampeni kwaiyo waumini wanajua na tumewaomba maana kuna wengine wanakua ni ngumu kupatikana siku za kawaida kwaiyo siku ileile ya ibada wakimaliza watakutana na mchanjaji yupo mlangoni na chanjo zake anawasubili wakimaliza ili aweze kuwachanja . Chanjo ni ileile inayotumika kwa njia za kawaida kwenye kampeni tunalenga kuwakusanya watu wengi Zaidi kwasababu kwenye kampeni haijalishi wewe mtoto wako alipata chanjo jana au juzi kwenye kampeni tunazoa wote chini ya miaka mitano.
Bi. Lotalias Gadau afisa mradi mpango wa Taifa wa chanjo wizara ya afya akitoa taarifa kwa waandishi wa habari umuhimu wa Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka mitano
Waandishi wa habari wakiendelea kufutilia taarifa ya chanjo ya Polio
Dr Bujite akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.

RC CHALAMILA AKAGUA UTENDAJI WA BANDARI BUKOBA (TPA)

MKUU wa Mkoa wa Kagera Alberth Chalamila amewataka watumishi wa bandari (TPA) kuwa waadilifu ,kuheshimiana, kuzingatia maadili na kutekeleza majukumu yao kama taratibu zinavyotaka hayo yamejili mapema mkoani hapo. "Mimi sehemu kubwa naangalia mapato ya umma hivyo nachoweza kusema Hapa bado hakuna utaratibu mzuri wa kibandari, uchakavu wa Miundombinu na matumizi sahihi ya teknolojia , kama bandari haina scanner ni jambo la hatqri , hili ni muhimu sana Meneja lishughulikie kwa nguvu na kwa uharaka Sana "ameeleza chamamila" Aidha ameeleza juu ya uholela wa mialo na upitishaji wa madawa ya kulevya na kuna mbinu nyingi zinatumika kupitisha madawa hayo ikiwemo kuweka kwenye nyama zinazoenda visiwani, pia upitishwaji wa mizigo ambayo hailipowi kwa kutopewa namba ya malipo mfano mizigo ya barafu na Mafuta hivyo kuwapa wiki Moja kabadilika kabla ya Kuanza kuchukua hatua kwani huduma wanayoitoa ni kwa manufaa ya umma.
Matukio ya Picha wakati ukaguzi unaendelea

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 31,2022

WAZIRI MASHIMBA NDAKI SERIKALI IMETENGA SH. BILLIONI 60 KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI

Na.Kadala Komba Dodoma SERIKALI imetenga sh.bilioni 60 kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuboresha shughuli zao, kuwaongezea mitaji na kuwapatia ajira ya uhakika. Hayo yamejili leo jijini Dodoma, na Waziri wa Uvuvina Mifugo Mashimba Ndaki wakati wa hafla ya kusaini makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi,vizimba vya samaki. “Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza wizara kuhakikisha kuwa uzalishaji wa samaki unaongezeka kutoka tani 497,567 na kufikia tani 600,000 ifikapo mwaka 2025. Aliongeza kuwa :”Kwa kuona fursa hiyo na kwa kuzingatia maelekezo na maagizo hayo katika mwaka 2022/2023 serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vyama vya ushirika, vikundi vya wavuvi, wakuzaji viumbe maji, wavuvi binafsi na makampuni ya wavuvi. Waziri alisema mikopo hiyo itahusisha zana za kisasa za uvuvi ikiwemo boti, nyavu, injini, vizimba, vifaranga vya samaki, chakula cha samaki na pembejeo za ukulima wa mwani. Ndaki alisema wizara ya mifugo na uvuvi kupitia sekta ya uvuvi watahakikisha kuwa mikopo hii inawafikia walengwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa ili kuongeza uzalishaji na kuongeza mchango wa Sekta ya Uvuvi kwenye pato la Taifa. “Natoa wito kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji kutumia mikopo hii kama ilivyokusudiwa na kuirejesha kwa wakati ili mkopo huu uweze kuwanufaisha wengine na kuwa endelevu. Sote tunafahamu kuwa, Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini. Alisema Kwa takwimu zilizopo, zaidi ya wananchi milioni 4.5 wameendelea kupata mahitaji yao kutokana na shughuli zinazohusiana na Sekta ya Uvuvi. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo (Uvuvi) Dk.Rashid Tamatama alisema serikali imekuja na mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuvikopesha vyama vyaushirika, vikundi vya wavuvi, wavuvi binafsi na makampuni ya wavuvi. Alisema watakopeshwa seti iliyotimia ya boti zenye urefu wa mita 7 hadi 14 zikiwa na injini zenye uwezo wa nguvu za farasi 9.9 hadi 60. Dk, Tamatama alisema boti hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba wavuvi sita hadi 20, kubeba Samaki tani 1.5, mtambo wa kufuatilia/kutambua uwepo wa Samaki , kifaa cha kuongoza boti , vifaa vya kuokolea Maisha na zana za uvuvi zikijumuisha mishipi na nyavu. “Jumla ya sh.bilioni 11.5 zitatolewa kwa ajili ya zimetengwa kwa ajili ya kukopeshwa na utalipwa kwa muda wa miaka mitano bila riba.pamoja na mkopo wa boti, Wizara pia itatoa mkopo kwa wafugaji samaki kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kujenga jumla ya vizimba 831 ambapo kila kizimba kimoja kitakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 144 M 3 – 256 M 3 . Katika hatua nyingine alieleza kuwa serikali itatoa vifaranga 4,080,000 na chakula cha Samaki tani 3,482.5. Aliongeza kuwa mkataba huo unaosainiwa utahusisha wakulima wa mwani ambapo wakulima 821 watakopeshwa kamba 108,372, tai tai 7,152,552 pamoja na mbegu za mwani. “Kwa ujumla kiasi cha sh.bilioni 21 zitatumika kwa ajili ya vizimba na zao la mwani,”alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki yak Maendeleo yak Kilimo (TADB) alisema watahakikisha mikopo hiyoinawafikia walengwa nakutoa matokeo chanya ya kuongeza mazao yatokanayo na uvuvi. “Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha hizi nyingi ambazo zinaenda kuwagusa wavuvi wa chini na kati na katika kuhakikisha mikopo yak fedha hiyo inatolewa kwa walengwa tumejipanga kuhakikisha inaenda kuwanufaisha,”alieleza Awali akitoa salamu za Bunge Mwenyekiti wa Kamati yak Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dk. Christine Ishengoma alisema kamati hiyo inampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuinua sekta ya uvuvi nchini. Alisemakatika kuhakikisha fedha hizo zinatumika pasipo ubadhilifu watahakikisha wanawatembelea mara kwa mara walengwa ili kuangalia namna mikopo hiyo itakavyo wanufaisha.
Waziri wa Uvuvina Mifugo Mashimba Ndaki wakati akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezajiwakati akizunguma katika
Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo (Uvuvi) Dk.Rashid Tamatama akitoa Utambulisho na Lengo la hafla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine akitoa neno la shukrani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha hizi nyingi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais - TAMISEMJ Dkt. Grace Magembe.
Mwenyekiti wa Kamati yak Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dk. Christine Ishengoma akitoa salamu za Bunge.
Matukio mbali mbali wakati kusaini mkataba wa makubaliano kati ya wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), kuhusu utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi,vizimba vya samaki.
Picha ya pamoja makundi mbali mbali

WAZIRI SIMBACHAWENE:AMEWATAKA WAKRISTO NCHINI KUFANYA KAZI KWA BIDII

Na Mwandishi wetu- Dodoma Wakristo nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujietea maendeleo, changia pato la Taifa na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma baada ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Askofu Donald Mtetemela kumaliza muda wake . Waziri Simbachawene alisema changamoto nyingi za kiuchumi katika jamii zitatatuliwa endapo wananchi watajituma kufanya kazi na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ambavyo maandiko matakatifu yanaagiza watu kufanya kazi. “Lazima wakristo wa sasa tufanye kazi lazima tutatue changamoto kwenye maeneo yetu maana imeandikwa katika biblia asiyefanya kazi na asile kwahiyo kufanya kazi ndio uhai wako, heshima yako na ukizalisha utaweza kuendesha maisha yako binfasi, utashiriki katika kazi ya Mungu na Taifa zima,” alisema Waziri Simbachawene. Pia aliongeza kwamba serikalii itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo, kusimamia maadili na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watu wasiyo na hofu ya Mungu. “Licha ya mchango mkubwa wa kanisa hili kwa serikali lakini kumekuwa na mmomonyoko wa maadili, magonjwa na majanga mbalimbali hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali ili kuokoa vijana na watoto wetu na ni matumaini yetu viongozi wa dini mkiendelea kusimama imara na kutoa huduma ya kiroho tutatatua changamoto hii,” alieleza. Aidha alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa , ufisadi, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma pamoja na jamii kwa ujumla. Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo Mndolwa aliipongeza serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuziunga mkono taasisi za dini katika nyanja zote huku akimtaka Askofu Chiteto kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu hatimaye kufikia malengo ya kanisa. Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutumia fursa ya serikali kushusha bei ya mbolea kwa kujikita katika kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Sherehe za kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.
Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Jijini Dodoma. Rev. George Chiteto (aliyelala) akiwekwa wakfu kuwa Askofu wa kanisa hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo Mndolwa akifafanua jambo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja baada ya ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya waumini wakifuatilia matukio mbalimbali katika ibada hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 30, 2022