Mchungaji na Mhubiri maarufu kutoka Tanzania Pastor Daniel Mgogo ametaja aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa mafundisho yake ndoa hizo haziwezi kudumu hata iweje.
Kwa mujibu wa Mchungaji Mgogo amesema ndoa lazima zibarikiwe na kiongozi wa kidini la sivyo ndoa hizo zitasambaratika tu. Mchungaji huyo alisema kuwa baadhi ya watu tayari wameoana bila ndoa zao kubarikiwa na sasa wanakimbilia kanisani kuwahadaa viongozi wa kidini ili kupata vyeti vya ndoa. "Msingi wa ndoa yako ni nini kama si uzinzi na uasherati? Na wakati mwingine mnatudanganya wachungaji, mnakuja mnasema tunataka kufunga ndoa. Kumbe mnataka kupata uhalali wa wizi wenu," Mgogo alisema.
Mhubiri huyo amewashauri vijana na wanandoa kuwa na subira na kufuata taratibu zote zinazohitajika kabla ya kufunga ndoa.
Pastor Mgogo aliwaasa wanandoa ambayo hawajaona kihalali kanisani kuweka wazi mahusiano yao kwa viongozi wa kidini na wakubali kuongozwa sala ya toba.
"Mchungaji awaongoze kwa sala ya toba. Awarudishe kundini abariki ndoa yenu, mfunge ndio mwende kwa mbwembwe. Mnakomaa na dhambi,Hamna hata aibu," Pasta Mgogo alishauri.
Home »
» MCHUNGAJI DANIEL MGOGO HIZI NDOA HAZIWEZI KUDUMU
MCHUNGAJI DANIEL MGOGO HIZI NDOA HAZIWEZI KUDUMU
Related Posts:
WAZIRI ULEGA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA MIZANI KUPISHA UCHUNGUZI Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa Mizani waliokuwa zamu katika Mizani zilizopo katika barabara kuu ya T1 ina… Read More
MBUNGE WA JIMBO LA BAHI MHE. KENNETH NOLLO AMSHUKURU MHE.RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO BAHI Na. Kadala Komba Bahi Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo kwa wananchi wa wil… Read More
MSAKO MKALI WALIOGUSHI VYETI VYA JKT Na. Angel Haule Dodoma Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao… Read More
ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI Na Mwandishi Wetu,, Kondoa MTU mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa bendera na mabango ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa mapokezi ya Ma… Read More
WANACHAMA WAPYA 20 WA CUF WAKABIDHIWA KADI Na Mwandishi Wetu, Kondoa MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara) Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua wa… Read More
0 Comments:
Post a Comment