Subscribe Us

TANROADS YATUMIA SHILINGI TRILIONI 1.37 KUKAMILISHA MIRADI 14 KWA KIPINDI CHA SERIKALI AWAMU YA SITA.

Na Moreen Rojas, Dodoma Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wenye gharama ya shilingi Trilioni 1.37. Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23. Mha.Mativila ametaja miradi hiyo ilivyokamilika kuwa ni miradi ya barabara ya Kidahwe_Kasulu (km 63) Mkoa Kigoma,Nyakanazi_Kibondo kabingo (km50) Mkoa Kigoma,Mbinga _Mbamba Bay (km66) Ruvuma,Njombe _Moronga section (km 53.9),Njombe Moronga_Makete section (km 53.30) Njombe Makutano _Natta(Sanzate)Section (km50) _Mkoa wa Mara Waso_Sale Jct section (km49)Arusha. Pia ametaja na Miradi ya madaraja makubwa iliyokamilika kuwa ni Tanzanite Bridge Dar_es_Salaam(km 1.03),Ruhuhu bridge along Kitai_Lituhi road in Ruvuma Region (m 98), Magara Bridge in Manyara region (m 84),Mara Bridge in Mara Region (m 940), Msingi Bridge Singida (m 100), Sibiti Bridge Singida (m 82), na Wami Bridge Pwani m 514. Aidha Mativila amesema kuwa jumla ya miradi 44 ya barabara yenye urefu wa kilometa 1,523 yenye gharama ya shilingi Trilioni 3.8 ipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi nchi nzima. "Miradi hii inahusisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa kupitia washirika mbalimbali wa maendeleo" Amesisitiza Mativila. Vilevile Mha.Mativila amesema kuwa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha msalato unaojumuisha ujenzi wa wa njia ya kurukia ndege na majengo ya abiria unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika(AFDB) kwa gharama ya shilingi Bilioni 360. Pia Mha.Mativila amesema kuwa miradi ya barabara 62 iko katika hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami. "Barabara hizi zinajumuisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani pamoja na fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo" Amesema Mativila. Ametaja miradi mingine kuwa ni Miradi ya EPC + F ambayo wizara ya ujenzi kupitia TANROADS imeanza utekelezaji wa miradi ya EPC + F yenye urefu wa kilometa 2,533 km, Makampuni yaliyokuwa "shortlisted" yamealikwa tarehe 22 September,2022 kuwasilisha zabuni tarehe 22 Novemba 2022. Katika mwaka wa fedha 2021/22 kati ya Julai 2021 hadi mei 2022 jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa Barabara na viwanja vya ndege inayogharamiwa kwa fedha za washirika na maendeleo ilisainiwa.
Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na vipaumbele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23.

0 Comments:

Post a Comment