Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo tarehe 12
Oktoba, 2022 amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA aliyoiteua hivi
Karibuni.
Akizungumza
katika hafla ya Uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya TAWA Mkoani
Morogoro, Dkt. Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa kumteua Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA na kuwapongeza wajumbe Wote wa
Bodi hiyo kuteuliwa kuiongoza TAWA.
"Nichukue
nafasi hii Kumshukuru sana Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumteua
"Chairman" (Mwenyekiti) wetu Mej. Jen.(Mstaafu) Hamis Semfuko asante
sana ametuletea "Chairman" hodari kabisa na Kwakweli tuna matumaini
makubwa sana na wewe" amesema
"Kwa dhati kabisa nawapongeza Wakurugenzi wa Bodi wote Kwa kuteuliwa kuiongoza Bodi hii ya TAWA" ameongeza.
Dkt.
Pindi Chana amesema uteuzi wa bodi hiyo umefanyika Kwa umakini mkubwa
na kuzingatia weledi na uzoefu wa wakurugenzi hao ambao utaisaidia
taasisi hiyo kufikia malengo hususani katika utekelezaji wa mikakati ya
kuzuia ujangili, kuongeza idadi ya watalii na mapato na hivyo kuendeleza
sekta ya Wanyamapori.
Aidha
Waziri Pindi Chana ametoa rai Kwa bodi hiyo Kuweka mikakati ya
Changamoto ya ongezeko la matukio ya Wanyamapori wakali na Waharibifu na
uvamizi wa mifugo hifadhini.
Sambamba na hilo, Mhe. Dkt. Chana amewataka watu wenye tabia ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kuacha vitendo hivyo mara moja.
"Nitumie
nafasi hii kuushirikisha Umma kwamba maeneo ya hifadhi zetu siyo maeneo
ya kulishia mifugo, haya ni maeneo ambayo tunapaswa kuyalinda Kwa
maslahi ya Wote" amesema
Dkt.
Chana ameongeza vitendo vya kuingiza mifugo hifadhini vinaleta athari
kubwa Kwa kukausha vyanzo vya maji, kuharibu mazingira na athari zake
kuwa kubwa Kwa Taifa, hivyo amewaomba wananchi washirikiane na Serikali
katika kuhifadhi maeneo yaliyohifadhiwa Kwa lengo la uhifadhi Kwa
maslahi ya Nchi yetu.
Mbali
na shughuli ya Uzinduzi wa Bodi, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alizindua
mitambo mbalimbali iliyonunuliwa na TAWA Kwa fedha za UVIKO - 19 ambayo
ni mashine za kuchima visima vya maji, matreka, "caterpillars", boti
maalumu kwa ajili ya doria n.k
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Elaimani Sedoyeka
amesema TAWA ina maeneo makubwa takribani asilimia 10 ya maeneo yote
Nchini, hivyo anatumaini kwamba itabuni mikakati mbalimbali ya kuongeza
idadi ya watalii, mapato na kuimarisha shughuli za Uhifadhi, kuboresha
miundombinu ya Utalii, kujenga uwezo wa watumishi pamoja na matumizi ya
teknolojia katika kuongeza ufanisi na tija kiutendaji.
Akielezea
mikakati ya Bodi mpya ya TAWA, Mwenyekiti wa Bodi Mej. Jen. (Mstaafu)
Hamis Semfuko amesema mkakati wa kwanza ambao Bodi itaupa kipaumbele ni
kupunguza migongano kati ya watu na Wanyamapori "Human Wildlife
Conflicts" Ili kuhakikisha TAWA inakuwa chombo ambacho kinakuwa na faida
Kwa Serikali na Umma.
Kamishna
wa Uhifadhi TAWA ambaye pia ni Katibu wa Bodi iliyozinduliwa leo,
Mabula Misungwi Nyanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Kwa kumteua Mej. Jen. Mstaafu Hamis Semfuko
kwa awamu nyingine Ili aendelee kufanikisha kazi kubwa aliyokwisha
ianzisha.
Aidha
amempongeza Mwenyekiti huyo Kwa kuendelea kuaminiwa na kuteuliwa
kuiongoza TAWA na kumuahidi ushirikiano Wakati Wote wa utekelezaji wa
majukumu ya Bodi Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
0 Comments:
Post a Comment