Subscribe Us

BILIONI 134.9 ZIMETENGWA KWAJILI YA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA

Na Moreen Rojas

Bohari ya dawa( MSD ) iliyopo chini ya taasisi ya wizara ya Afya imepokea shilingi Bilion 134.9 Kati ya shilingi Bilion 200 zilizolengwa kwa manunuzi ya bidhaa za afya kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Hayo yamesemwa na Mkurugezi mkuu wa bohari ya dawa ( MSD) Mavera Tukai wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma juu ya maboresho ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Amesema bohari ya dawa imetekeleza majukumu manne ambayo ni uzalishaji,utunzaji na usambazaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya pamoja na vituo binafsi vilivyohizinishwa na wizara ya Afya.

Mpaka sasa vituo vya kutolea huduma za Afya ni 7, 153 inchi zima kupitia kanda 10 zilizopo Dodoma, Dar -es- salaam, Mtwara, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Tanga, kagera mbeya na Iringa.

Aidha Amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 bohari ya dawa imeendelea kufanya maboresho ya utekelezaji kama ilivyoelezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambayo  mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya na utawala bora.

" Maitaji yanayotekelezwa kwa sasa  ni kuingia mikataba ya muda mfupi na wazalishaji wa bidhaa za afya,kufanya mapitio ya ununuzi wa bidhaa za afya , kufanya mapitio ya mabadiliko ya  matokeo ya bidhaa  za afya, kufanya matukio ya usimamizi wa mali pamoja na kuimarisha ushirikiano wa wateja na wadau wa sekta nyingine za afya"Amesema Tukai.


Pia Tukai amesema usambazaji wa bidhaa za afya ufanyika mara 6 kwa mwaka ambapo kila kituo upelekewa bidhaa za afya kila baada ya miezi miwili kwa mujibu wa kalenda ya usambazaji Pamoja na kuimalisha upatikanaji wa dawa hadi kufika 90%.

Mwisho.
 

 

 

0 Comments:

Post a Comment