Na Moreen Rojas Dodoma
Vijana
wengi wameingiwa na hofu ya kukataa kuchanjwa chanjo ya uviko 19 kwa
kuhisi watapunguza nguvu za kiume pamoja na kuhisi watajiingiza katika
imani za kishirikina.
Hayo
yamesemwa na Bi.Flora Kimaro mratibu msaidizi wa chanjo jiji la Dodoma
wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya na waandishi wa
habari uliofanyika katika hotel ya nala jijini Dodoma.
Aidha
ameongeza kuwa vituo vya afya zaidi ya 65 vinaendelea kutoa chanjo ya
uviko 19 katika jiji la Dodoma ambapo kiuhalisia watu wazima ndio
wanaochanja zaidi,waliowengi wanaochanja ni wazee na sio vijana "Amesema
Bi Kimaro.
Mikakati
ambayo Serikali inayo ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na
sasahivi ni kupita nyumba hadi nyumba kuendelea kuelimisha jamii kuhusu
uviko 19 " Amesema Bi Kimaro.
Kwa
makundi hatarishi jiji la Dodoma wameyafikia kwa kiasi kikubwa sana kwa
wanaoishi na HIV,TIB na Kisukari ambayo kinga zao zinashuka kwa hiyo
wameendelea kuyafuatilia ikiwemo wazee ambao kinga yao ya mwili imeshuka
"Amesema Bi Kimaro.
Ameongeza
kuwa endapo tutafikia asilimia 80% kama nchi zingine zilizofanikiwa
hakutakuwa na umuhimu wa kuzingatia uviko 19 ikiwemo suala zima la kuvaa
barakoa kwani tutakuwa tumejikinga kwa eneo kubwa " Amesema Bi Kimaro.
Kwa
upande wake shuhuda wa kwanza wa chanjo ya uviko 19 Jane Shemndolwa
ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata kutoka halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa
kata ya Chitemo amesema kuwa alikuwa haamini kwenye kuchanja kutokana
na maneno kwamba ukichanja unageuka kuwa zombi,kama kiongozi kwenye
jamii ameamua kuchanja ili kuwa mfano kwa jamii yake ili waweze
kuhamasika kuchanja na binafsi hajawahi kupata madhara yoyote "Amesema
Shemndolwa.
Shuhuda wa
pili wa chanjo ya uviko 19 Jovery Tairo ambaye ni mwakilishi wa
mchungaji kutoka kanisa la M.R.B Prophetic Ministry amesema kuwa kwake
ilikuwa ngumu kama kijana mwenye imaani kupata chanjo ya uviko 19 kwani
walikuwa wakiambiwa kuwa ni mpango wa kishetani wa kupunguza watu lakini
baada ya kuhudhuria semina amepata elimu ya chanjo na ameona mambo hayo
hayahusiani na chanjo nakuwashauri vijana kujitokeza waweze kupata
chanjo " Amesema Tairo.
Naye
Mwenyekiti wa mafunzo Shekhe.Musa Kalasa amesema alichanja kwa utata
sana kwa sababu alikuwa anafikiri ukichanja damu inaganda,lakini
alipopata elimu akaona hizi ni fikra tu fikra kama hizi zipo lakini yeye
amekuwa balozi kwa waumini wake wanaume kwa wanawake, ikiwa Rais Samia
ameweza kuchanja na damu haijaganda mimi ni nani nisichanje? "Amesema
shekhe Kalasa.
Wanachi
wameendelea kuhamasishwa kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa uviko 19
ikiwemo kuchanja chanjo zote ili kupunguza kasi ya ugonjwa huo.
Bi.Flora Kimaro mratibu msaidizi wa chanjo jiji la Dodoma
wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya na waandishi wa
habari
Waandishi wa habari wakipatiwa mafunzo namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko 19 |
|
0 Comments:
Post a Comment