Na. Kadala Komba Dodoma
Malalamiko ya wafanyakazi wa kampuni ya
uchimbaji Madini BARRICK ambao waliachishwa kazi Kwa nyakati tofauti
kuanzia mwaka 2007 Serikali imebainisha hatua zilizochukuliwa katika
kushughulikia malalamiko hayo.
Malalamiko
hayo yalihusiana na wafanyakazi kutopimwa afya wakati wa kuachishwa
kazi, kutopatiwa huduma ya matibabu na kutopewa malipo ya fidia kutokana
na ajali au magonjwa waliyoyapata kutokana na kazi.
Akizungumza
na na waandishi wa habari Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana
Ajira na wenye ulemavu Prof.Juma Katundu amesema kuwa Malalamiko hayo
yameshughulikiwa katika hatua mbali mbali, kupitia Wakala wa Usalama na
Afya mahali pa kazi (OSHA), Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Idara
ya Kazi. Hata hivyo, wafanyakazi hao waliendelea kuwasilisha malalamiko
katika mamlaka mbalimbali za Serikali wakidai kutoridhishwa na hatua
zilizochukuliwa.
"Kutokana
na hali hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu ilichukua hatua mbalimbali za kiutawala (administrative
measures) ili kuyapatia ufumbuzi malalamiko hayo,
"Hatua
hizo ni pamoja na kuunda Timu Maalum mwaka 2021 na 2022 zilizojumuisha
wataalam kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali, Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE) kwa lengo kufanya uchambuzi wa kina wa malalamiko ya wafanyakazi
hao na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuyahitimisha,"amesema.
Aidha
amesema kuwa timu husika zimeshughulikia jumla ya walalamikaji 427,
kati yao walalamikaji 150 walishughulikiwa mwaka 2021 na 277 mwaka 2022,
hata hivyo, kati ya walalamikaji 277 wa mwaka 2022, walalamikaji 47
walishashughulikiwa na timu ya mwaka 2021.
"mwaka
2022, kabla ya timu kuanza kazi, mwezi Mei, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ilitoa tangazo kupitia Vyombo vya
Habari kuwataka waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick wenye
malalamiko ambayo hayajawahi kuwasilishwa na kutolewa maamuzi na vyombo
vya Serikali, kuwasilisha malalamiko yao ili yafanyiwe kazi,
Timu
iliyoundwa imekamilisha uchambuzi na kuwasilisha taarifa kwangu,Katika
taarifa hiyo imeainishwa kuwa wapo walalamikaji waliobainika kuwa na
magonjwa yanayotokana na kazi na hivyo mwajiri atawajibika kuwapatia
matibabu, wapo wenye magonjwa yatokanayo na kazi na wamefikia ukomo wa
kuimarika afya zao na hivyo mwajiri atatakiwa kuwafanyia taratibu za
kuwalipa fidia. Vilevile, wapo waliobainika kuwa na magonjwa
yasiyotokana na kazi,"alifafanua.
Pia
amesema kuwa Kwa kuzingatia matokeo hayo, walalamikaji wote
waliowasilisha malalamiko yao watapatiwa majibu yao kwa barua ndani ya
siku kumi za kazi baada ya kutoka tangazo hili.
Amesema
barua hizo zitatolewa kupitia Ofisi za Idara ya Kazi za Mikoa au Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kwa kutumia anuani walizobainisha katika
barua zao za malalamiko,Aidha, yeyote ambaye atapenda kupata barua kwa
njia tofauti na zilizoelezwa, awasiliane na Ofisi ya Kamishina wa kazi
kupitia namba ya simu 0655 544 489.
"Ninapenda
kutoa taarifa kuwa nimemtaka mwajiri kuweka Dawati/Ofisi maalum kwa
ajili ya kusikiliza na kutatua malalamiko na kero za wafanyakazi,
Nimearifiwa
kuwa Mwajiri ameshatekeleza agizo hilo, ambapo amefungua Ofisi maalum
katika eneo la Boomgate Bulyankulu (Nje ya mgodi). Hivyo, niwatake wale
wote wenye malalamiko dhidi ya Kampuni ya Barrick kufika katika
Dawati/Ofisi hiyo kuwasilisha malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa
kazi,Aidha, Uongozi wa Kampuni uandae utaratibu wa namna ya kupokea
malalamiko kwa kutoa namba ya simu maalum na watumishi ambao
watashughulikia malalamiko,"amesema.
Pia
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya kazi, Wakala wa Usalama na Afya
Mahali Pa Kazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) zitaendelea
kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi nchini kwa mujibu wa Sheria za
Kazi.
Aidha, Ninapenda
kuchukua fursa hii kuwakumbusha Waajiri wote nchini kuwa Wakala wa Afya
na Usalama Mahali Pa Kazi (OSHA) ndiyo yenye mamlaka kwa mujibu wa
Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Na. 5 ya 2003 ya kupima afya za
wafanyakazi ili kubaini endapo wana madhara yaliyosababishwa na kazi
wanazofanya.
"Ninatoa rai
kwa waajiri na wafanyakazi katika Sekta ya Madini kutekeleza wajibu na
majukumu yenu kwa Uadilifu na kufuata misingi ya kitaaluma kwa lengo la
kudumisha Mahusiano mema pahala pa kazi na hivyo kuepuka kuwepo kwa
malalamiko na migogoro isiyo ya lazima ili kujenga nguvu kazi shindani
na Maisha bora,"ameeleza.
0 Comments:
Post a Comment