Na. Kadala Komba Dodoma.
IMEBAINISHWA
kuwa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan za kuitangaza nchi pamoja na vivutio vilivyomo kupitia filamu
maalum ya Royal Tour matokeo chanya ya filamu hiyo yameanza kushuhudiwa
katika mwaka wa fedha wa 2021/22 katika kiwanja Cha Kilimanjaro
International Airport (KIA).
Miongoni
mwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la abiria kutoka laki 347,757
mwaka 2020/21 na kufikia abiria laki 654,159 mwaka 2021/22 ni sawa na
ongezeko la asilimia 88.
Hayo
yameelezwa Leo Oktoba 11 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa kampini
ya uendelezaji na uendeshaji wa kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KIA)
wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za KADCO kwa vyombo
vya habari.
Amesema kuwa
mafanikio mengine ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings
Discover(part of Lufthansa Group)iliyoanza safari zake kutoka
Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo
linachangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.
"Kuendelea
kuwa na mashirika mbalimbali ya ndege za kukodi(charter flights)ambayo
yameendelea kutumia KIA kwa kuleta makundi maalumu ya watalii kutoka
sehemu mbalimbili duniani,
Kuvutia
wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi kuwekeza KIA katika maeneo
tofauti ikiwemo hotel za kisasa,maeneo ya biashara mchanganyiko(business
Complex)na jengo la wageni mashuhuri(CIP lounge facility),"Ameeleza.
Kadhalika
amesema kuwa jali ya uendeshaji uliendelea kuimarika hadi mwaka wa
fedha 2020/21 ambapo Dunia ilikumbwa na janga la Uviko 19 lililoathiri
sekta nyingi za kiuchumi Duniani ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri wa
anga.
Amesema katika
kipindi hicho shughuli za uendeshaji KIA zilishuka kwa kiasi kikubwa
kutokana na nchi nyingi kufunga anga ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia
kusambaa kwa ugonjwa huo,hii ilipelekea idadi ya abiria kushuka kwa
kiwango kikubwa kutoka laki 794,337 mwaka 2019/20 hadi kufikia abiria
laki 347,757 katika kipindi Cha mwaka 2020/21 ikiwa ni punguzo la
abiria kwa asilimia 56.
"Kupunguza
kwa shughuli za uendeshaji KIA kuliathiri mapato,ikizingatiwa kwa
chanzo kikuu Cha mapato ya KADCO ni tozo zinazotokana na abiria
wanaopita KIA pamoja na kutua na kuruka kwa ndege kiwanjani,hali hii
ilipelekea menejimenti ya KADCO kuchukua hatua ya kubana matumizi na
kusimamisha kwa muda baadhi ya shughuli za maendeleo ili iweze kupita
Katika kipindi hiki kigumu ikiwa inaendelea kujiendesha,
Hata
hivyo nikiri kuwa kipindi hiki tukiendelea kutoa huduma kwa kukidhi
viwango vya kitaifa na kimataifa wakati wa janga la Uviko-19 na
kutambuliwa kama moja ya viwanja kilichofanya vizuri zaidi katika
kipindi hicho kwa kuzingatia maelekezo ya kujikinga yaliyokuwa
yanatolewa kupitia Wizara yetu ya Afya,"amefafanua.
Ikumbukwe
kuwa Usafiri wa anga ni chachu ya kuwezesha kukua kwa sekta nyingine
mtambuka ikiwemo sekta ya Utalii, mifugo,kilimo na biashara ambapo
huimarisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani
unaotokana na shughuli za uendeshaji wa KIA,mazao mbalimbali ya kilimo
na mifugo hupitia KIA kwa ajili ya kwenda kwenye masoko ya nje ya
nchi,hii inafaida kubwa katika uchumi wa kanda ya kaskazini na Taifa kwa
ujumla.
Mwisho
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa
kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine
Mwakatobe,akizungumza na waandishi wa habari
0 Comments:
Post a Comment