Na. Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Hospitali ya Benjamin Mkapa
Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo Oktoba 13, imetimiza miaka saba tangu ilipoanza kutoa huduma za Afya Oktoba 13, 2015.
Mkurugenzi
Mtendaji Dkt, Alphonce Chandika amewajengea uwelewa juu ya Msuada wa
Sheria ya Bima ya Afya kwa wote wananchi waliyofika kupata huduma,
ambapo mesema lengo la Mswada huo ni kuhakikisha, kila mwananchi
anakuwa na uhakika wa kupata matibabu bila hofu.
“Ndugu
zangu baadhi yenu mnakuja hapa mara kwa mara kupata huduma, mnafahamu
ugonjwa haubishi hodi, bila kuwa na BIMA kuna wenzetu hulazimika kuuza
hata viwanja au nyumba wagharamie matibabu” Alidokeza, Dkt. Chandika.
Aidha,
alifafanua kuwa mantiki ya Mswaada wa BIMA ya Afya kwa wote ni
kuhakikisha kuwa, watu wengi wanachangia gharama za matibabu kabla
hawajafikwa na maradhi ili kutunisha mfuko hatimae mtu akiugua asikutane
na changamoto yoyote ya kukosa huduma kwa kushindwa kulipia gharama za
matibabu.
“Msingi
wa BIMA ya Afya kwa wote, ni suala la upendo zaidi, na baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere tunaeadhimisha siku yake kesho alitufundisha kupendana,
hivyo tunapochangia wengi, wakaugua baadhi tunakuwa tumewasaidia”
Alifafanua Dkt. Chandika.
Vile
vile, alieleza kuwa mapendekezo ya Mswada huo ni kwa kaya moja
kuchangia Shilingi 340,000 na kunufaisha wanafamilia sita, huku mtu
mmoja akitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 84,000 ili kupata huduma za
Afya kwa mwaka mzima.
“Nasisitiza
kuwa serikali haina lengo la kumlazimisha mtu kuchangi, bali itaweka
mazingira rafiki yatakayomsukuma kila mmoja kuona umuhimu wa kuchangia,
na kwa kutumia mifumo ya TASAF na Ustawi wa jamii itawatambua
wasiyojiweza na kuwatengenezea mfumo wa kupata matibabu bila usumbufu”
Alisema Dkt. Chandika.
Shamrashamra
za kutimiza miaka hiyo saba zimeanza saa mbili asubuhi ya leo kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika kushiriki
kutoa huduma za msingi kwa wagonjwa, aliwapokea, kuzungumza nao na
kuwasaidia waliyohitaji kutembea kwa msaada wa kiti maalumu
(Wheelchair).
Kisha
aliwashukuru wananchi waliyofika Hospitalini hapo kwa kutoa mchango wao
wa maoni, ambayo hupokewa na kufanyiwa kazi kwa wakati na ndiyo umekuwa
msingi wa maboresho mbalimbali ya huduma katika Hospitali hiyo kiasi
cha kuifanya kutambuliwa kama kinara kwa Utoaji wa huduma bora za Afya
kwa Hospitali zote nchini.
Kwa
asubuhi ya leo, sherehe hizo ziliahanikizwa na ukataji wa keki maalumu
ya miaka saba ya huduma katika Hospitali hiyo, ambayo ilikatwa kwa
ushirikiano wa Mteja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
Baadaye alielekea katika wodi ya watoto wachanga na kutoa zawadi mabalimbali kwa watoto hao kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Dkt, Alphonce Chandika akizungumza na wanainchi waliyofika kupata huduma juu ya Msuada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.
0 Comments:
Post a Comment