Subscribe Us

BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO NCHINI [CPB] IMEWATOA HOFU WAKULIMA WA MAZAO YA KUNDE


 

Na. Mwandishi wetu Simiyu

 

Bodi ya mazao mchanganyiko nchini (CPB) imesema kuwa wakulima nchini wenye mazao aina ya kunde, hawana sababu ya kuhangaika na soko la mazao yao kwani Bodi hiyo inao uhitaji mkubwa wa mazao hayo.

Ofisa Masoko wa Bodi hiyo Frank Bubelwa Akizungumza katika maonyesho ya wiki ya Chakula nchini yanayoendelea Mkoani Simiyu, amesema kuwa wakulima hawana sababu ya kuangaika na kutafuta wapi watauza mazao yao. Amesema serikali kupitia wizara ya kilimo, mazao na nafaka tumeona tuingie, tufungue milango kwa wakulima kwa kuweza kununua mazao yao yote ambayo wanalima na kuleta kwetu sisi inamaana kwa lugha nyepesi tunawasaidia kutoka katika changamoto ambayo walikuwa wananung’unika kupata masoko.

 

Aidha ameongeza kuwa mbali na Bodi hiyo kununua mazao kutoka kwa wakulima, bado bei ambazo wamekuwa wakinunulia mazao hayo ni rafiki kwa wakulima Lakini pia katika swala zima la bei za nafaka sisi kama taasisi sio taasisi kandamizi mkulima anapewa fursa na tunampa fedha inayoendana na bei ya sokoni mara nyingi wakulima wanakuwa na changamoto hiyo kubwa, unakuta mkulima anakuja kudalaliwa na mtu wakati kwa bei ya chini ambayo inamfanya yeye hasipate hamu au mtaji wake unaguswa kwaiyo anashindwa kufanya shughuli za kilimo. Sambamba na hilo afisa masoko Frank Bubelwaa amesema  kuwa katika msimu wa kilimo bodi ya nafaka huwa tunaangalia pande zote mbili mkulima hasiumie pia sisi tusipate hasara kwaiyo mara nyingi tunanunua mali kutokana na bei iliyo sokoni kama kwamfano kilo moja ya mahalage ni silingi elfu mbili sokoni sisi tutakuja kununua kwa bei hiyohiyo hatuwezi tukashuka Zaidi ya hapo. Hivyo basi sisi tupo kwaajiri ya kuhakikisha kuwa kilimo kinaendelea kukua lakini pia kwaupande mwingine kuongeza uchumi wa nchi.

 

maonyesho ya wiki ya Chakula nchini yanayoendelea Mkoani Simiyu
 

 

 

 

 

 

 

0 Comments:

Post a Comment