Na Mwandishi wetu Kigoma
Naibu
Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea Mradi wa
Kuboresha Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma. Mradi huu
unatumia ziwa Tanganyika kama chanzo cha maji, katika eneo la fukwe ya
Amani, Kata ya Bangwe Kigoma.
Mhe.
Mahundi amesema hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo
inatia matumaini, na amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
mazingira Kigoma (KUWASA) kuhakikisha inafuatilia kwa karibu ujenzi wake
kwa mkandarasi ili mradi huo ukamilike mapema ili wananchi wapate
huduma.
Amesema
nia ya serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya
majisafi na salama. Aidha, amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya
Kigoma Ujiji pamoja na Mji mdogo wa Mwandiga wasiwe na mashaka. Maji ya
kutosha yanawafikia muda sio mrefu.
Awali
akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Kigoma Mhandisi Mbike Jones amesema mradi huo
unatarajia kukamilika Desemba 2022 na utaweza kuhudumia wananchi zaidi
ya 280,000 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na mji mdogo wa Mwandiga.
Amesema kwa sasa mahitaji ya wananchi wa maeneo wanayoyahudumia ni lita za ujazo Milioni 24 kwa siku wakati mradi huo unatarajiwa kuzalisha lita milioni 42 kwa siku. Gharama ya mradi huo inatarajiwa kufikia Euro 16,323,152.67 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 42 ikiwa ni ufadhili kutoka Jumuia ya Ulaya (EU)#SHINENEWSBLOG
0 Comments:
Post a Comment