Na. Kadala Komba Dodoma
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya amewataka
wazazi kuwapeleka watoto shule badala ya kuwapa kazi ya kuchunga
Ng'ombe .
Askofu huyo aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa misa
ya Sakramenti ya kipaimara iliyofanyika katika kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Wilaya ya Bahi.
Amesema
elimu bora ni haki ya kila mtoto ambapo hatua hiyo itasaidia watoto
kutimiza ndoto zao pamoja na kuongeza pato la familia na kuondokana na
umasikini.
"Ni kweli
hizi familia zina utajiri wa mali nyie ni wafugaji wa mifugo na kupitia
mifugo mnamiliki mali nyingi lakini mali bila elimu ni shida, wapelekeni
watoto shule wakapate elimu darasani, wafundisheni watoto kusoma pindi
wanapokuwa Nyumbani, "Alisema Askofu huyo.
Pia
Askofu Mhashamu aliwasihi watoto kutumia vizuri fursa ya elimu
wanapopelekwa shule kwa kusoma bidii kusoma kwa bidii na kutokukubali
kukatishwa tamaa.
Katika
hatua nyingine Askofu alipongeza Parokia hiyo kwa juhudi za kimaendeleo
ambazo Parokia inaendelea kufanya uhakikisha jamii inakuwa na hofu ya
Mungu na maadili.
"Parokia
hii inakuwa kwa kasi hivyo msikubali kukatishwa tamaa na watu, msije
kugeuka nyuma ukigeuka nyuma utakuwa jiwe la chumvi hivyo tunatakiwa
kutazama tulijenge Kanisa, "Alihimiza.
Kwa
upande wake Katibu wa Halmashauri ya Walei Parokia, Eresta Oiso
ameeleza kwamba jumla ya watoto 1,776 wamepata Sakramenti ya ubatizo,
komunio ya kwanza 329 na ndoa 71 zilifungwa pamoja na kutoa Sakramenti
ya kipaimara kwa watoto 301 pamoja na kufungisha ndoa 5.
"Parokia
ya Bahi ni miongoni mwa Parokia zilizomo ndani ya Jimbo Kuu Katoliki
Dodoma, Dekania ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji inapatikana mpakani mwa
jimbo kuu Katoliki Dodoma na jimbo la Singida takribani kilomita 55
kutoka Dodoma mjini, "Ameeleza.
Aidha amebainisha kuwa Parokia ya Bahi ina Jumla ya vigango 13 , Vigango 11 na jumuiya ndogo ndogo za kikristo 155.
MATUKIO YA PICHA YA KIPAIMARA
0 Comments:
Post a Comment