Subscribe Us

WATOTO YATIMA WAIOMBA BAKWATA KUWAWEKEA UZIO

 

Na Peter Mkwavila KONDOA

WATOTO wa Kituo cha yatima kinachomilikiwa na taasisi ya All Hafidhu Islamic Orphans Centre kilichopo Bicha wilaya ya Kondoa.

Wameliomba Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuwajengea uzio utakao wawezesha kudhibiti uharibufu wa vibaka ikiwemo na ulinzi wa mipaka ya kituo hicho  na jamii inayowazunguka.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Ukht Aisha Nobe,kwa niaba yao watoto mbele ya Shekhe wa mkoa wa Dodoma (BAKWATA) Mustaph Rajabu wakati alipokuwa akifunga kongamano la wanawake wakiislamu la siku 3 lililofanyika kituoni hapo.

Aisha,alisema kituo hicho kwa muda mrefu toka kujengwa hakina uzio ambao unaoweza kudhibiti vibaka na hata mipaka ya maeneo yanayozunguka.

“Mbali na kituo hicho kuwa na wanafunzi wa shule ya msingi,pia tunawatunza watoto wenye mahitaji maalumu,ila hakuna uzio ambao unaoweza kulinda mipaka na usalama wa mali na wao wenyewe”alisema.

Akizungumza kwenye kongamano hilo lililowashirikisha wanawake kutoka dini ya kiislamu  kwa ajili mafunzo,pia maada mbalimbali zilitolewa ikiwemo ya elimu kwa wanawake,malezi kwa watoto ndoa,ibada na ndoa ya mitaala.

Kwa upande wao washiriki ambao ni wanawake wametakiwa kuwa mabalozi wa elimu waliyoipata kwa wengine ili dini hiyo iweze kuondokana na changamoto zinazowakabiri.

Naye Shekhe wa Mkoa wa Dodoma wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mustapha Rajabu,alisema Kituo hicho kinatakiwa kuwa kwenye usalama zaidi ukizingatia kuna watoto wadogo wanaohitaji usalama mkubwa.

Alisema kutokana na umuhimu huo Bakwata kwa kushirikiana na taasisi zingine na wadau wa elimu watahakikisha wanasaidia kuondoa kero hiyo ya kukosa uzio ambao umesababisha kuwepo kwa mwingiliano.

“Nimesikia kilio chenu sisi kama Bakwata tutahakikisha tunashirikiana na wadau wengine tunatatua kero hii ili watoto wetu wasome kwenye hali ya usalama na hata mali zao ziwe salama pia na hata kwenye mipaka nayo ijulikane pia”alisema.

MWISHO.

 

 


 


0 Comments:

Post a Comment