Na. Mwandishi wetu Morogoro
Serikali
Kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kutumia
teknolojia ya kufuatilia mienendo ya wanyamapori katika maeneo ya
hifadhi kwa kuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kutambua mienendo ya
wanyamapori mbalimbali wakiwemo wale walio hatarini kutoweka na
wanaosababisha migogoro kwenye jamii.
Kauli
hiyo imetolewa leo mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokua akizindua zoezi la Kuvisha
Mikanda yenye Redio za Mawasiliano kwa wanyamapori linalofanywa na
Watalaam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania ( TAWIRI)
lililofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo jumla ya makundi
53 ya wanyamapori yanatarajiwa kifungwa mikanda hiyo nchi nzima.
"Katika
kufuatilia mienendo ya wanyamapori waliohatarini kutoweka, teknolojia
hii husaidia kutambua uwepo wao, mienendo na mtawanyiko katika mifumo
ikolojia yao. Utambuzi huu husaidia katika kuimarisha nyanda za malisho
na ulinzi." amesema Balozi Dkt . Chana
Amesema
kwa upande wa wanyamapori waharibifu, teknolojia hiyo husaidia kutambua
makundi na mienendo yao na kutoa taarifa mapema kuhusu uwepo wa
makundi hayo nje ya hifadhi na kichukua hatua kabla ya hayajasababisha
madhara.
"Taarifa hizi husaidia katika kupanga mbinu muafaka za kukabiliana na wanyamapori hao. " amesisitiza Balozi Dkt. Chana
Katika
hatua nyingine ameeleza kuwa zoezi hilo alilolizindulia limelenga
kuimarisha uhifadhi na utalii kusini mwa Tanzania hususan katika Hifadhi
za Taifa za Nyerere, Ruaha na Mikumi akifafanua kuwa litasaidia kwa
kiwango kikubwa katika kupunguza migogoro baina ya jamii zinazozunguka
hifadhi. "Jumla ya makundi ya wanyamapori 53 yatafungwa mikanda hii
yenye redio za mawasiliano katika hifadhi hizi tatu." amesisitiza Balozi
Dkt. Chana
Sambamba na
hayo, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameongeza kuwa wanyamapori
watakaofungwa mikanda hiyo ni pamoja na makundi ya tembo, simba, chui,
duma, mbwa mwitu na twiga.
Aidha,
taarifa na takwimu hizo zitasaidia kuandaa ramani za mitawanyiko ya
wanyamapori katika misimu na nyakati mbalimbali ambazo zitasaidia
kufungua njia mpya za utalii “tourism circuits” pamoja na kuimarisha
uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi hizo.
Naye
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amesema
Tekinolojia hiyo itasaidia kuwalinda Wanyamapori na Hifadhi zetu hapa
nchini. Pia, itasaidia kufuatilia mienendo ya Wanyamapori hai na kuweza
kuwaona kidijitali pindi wanapotaka kuleta madhara.
"Kwa
kutumia tekinolojia hii tunaweza kuwaona kidijitali wanapotembea na
hasa wanapokaribia maeneo hatarishi ya kuleta madhara kwa wananchi"
0 Comments:
Post a Comment