Na Kadala Komba- Dodoma
Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu amewataka wanafunzi kusoma kwa juhudi na kujiamini ili kufanya vizuri katika mitihani yao hatimaye waweze kujiunga na masomo ya elimu ya juu.
Diwani huyo ameyasema hayo hivi karibuni katika mahafali ya 11 ya kidato cha nne shule ya Sekondari Mpamatwa iliyopo Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma ambapo alisema Serikali ya Awamu za Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imefuta ada kuanzia chekechea hadi kidato cha sita hivyo ni jukumu la wanafunzi kusoma kwa bidii.
Amesema kupitia mfuko wa Wilaya wa kusomesha watoto wanaotoka mazingira duni kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha tano mradi unatoa fedha ya kijikimu kwa mtoto, magodoro, madafutali pamoja na nauli ya kwenda shuleni.
"Nendeni mkafaulu mitihani yenu vizuri kwani Wilaya hii ina mfuko wa Wilaya wa kusaidia watoto wenye hali duni (KOIKA), na Mimi ndiye Mwenyekiti wa mradi huo hivyo nawaomba mfanye vizuri kidato cha nne ili mradi uweze kukutimizia ndoto zako, kwa sababu usipofanya vizuri na ukafaulu , ufaulu wa kati tafsiri yake utampa mzigo mzazi kukupeleka chuo kwani chuo ni gharama kubwa,” Amesema Diwani huyo.
Vivile vile Diwani Mpandu ameeleza kwamba Kata hiyo ina shule za msingi tano huku akieleza kuwa matarajio yao ni kuwa na shule za Sekondari sita na zoezi hilo tayari limeanza Bahi makulu, ili waweze kuwa na shule yao kuwasaidia wanafunzi kuepuka kutembea umbali mrefu kufika shuleni hivyo ni lengo letu Bahi iwe ya mfano kwa kuwa na shule za sekondari nyingi na shule nyingi za msingi.
"Kwa mwaka huu mradi umewapeleka wanafunzi 35 shule katika Wilaya yetu ya Bahi waliyofanya vizuri kupitia mfuko huu, ndiyo maana nasema wanafunzi nendeni mkafanye vizuri kwenye mitihani yenu,nawaomba msiniangushe mfano kuna kijana anaitwa Deogratius Malula alifanya vizuri sana mwaka jana akapata division one amekuwa mfano mzuri kwa ufaulu wake na sisi kupitia mfuko tumeweza kumsaidia,” Amebainisha.
Aidha Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Joyce Manyanda amesema elimu sio lele mama hivyo wanafunzi hawana budi kujiamini pindi mnapokuwa katika chumba cha mitihani pamoja na kuwahimza wanafunzi kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani pindi wanapokuwa likizo.
"Juhudi msiziweke katika masomo tu pia mfanye kazi za nyumbani wakati wa likizo msaidie wazazi na walezi wenu kufanya hivyo kutawajenga pia watoto wasaidieni wazazi kazi za nyumbani kipindi cha likizo kufanya hivyo kutawajenga kujitegemea siku zijazo,”Amesisitiza Bi. Joyce.
MWSHO
Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu akizungumza katika mahafali ya 11 ya
kidato cha nne shule ya Sekondari
Mpamatwa
0 Comments:
Post a Comment