Na. Moreen Rojas, Dodoma.
Taasisi
ya Afrika ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela inadhamiria
kupendekeza ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike wenye watoto wadogo na
mahitaji maalum ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.7 zimetumika katika
ujenzi huo.
Hayo
yamesemwa na Makamu Mkuu wa chuo Prof.Emmanuel Luoga wakati akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali
zinazotekelezwa na taasisi hiyo.
Prof.Luoga
amesema kuwa wameamua kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike wenye watoto
wadogo na wenye mahitaji maalumu ili kuwawekea mazingira wezeshi
yatakayowasaidia kusoma bila changamoto yoyote ambapo bweni hilo
litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 pindi awamu zote tatu za
ujenzi utakapokamilika.
Aidha
ameeleza kuwa wanafunzi wa kike wanapoingia vyuo vikuu kwa ajili ya
shahada ya pili au ya tatu wanakuwa tayari wameshaanza majukumu ya
kifamilia kwahiyo bweni hilo litasaidia kukidhi mahitaji yao.
Prof.Luoga
ameongeza kuwa kipaombele kingine cha taasisi hiyo ni kuimarisha mifumo
ya tehama katika chuo hicho na kuangalia uwezekano wa kuandaa wataalam
watakaosaidia taifa katika kutoa elimu ya masafa ili kukabidiliana na
upungufu wa walimu wa sayansi hapa nchini.
Taasisi
ya afrika ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela ilianza rasmi
kudahili wanafunzi mwaka 2021 na kujikita katika kufanya utafiti na
ufundishaji katika ngazi ya uzamiri na uzamifu ambapo katika mwaka huu
wa fedha 2022/2023 serikali imetenga zaidi ya bilion 42 zitakazo tumika
kwa ajili ya mishahara na matumizi mengine pamoja na miradi ya
maendeleo.
Mwisho.
0 Comments:
Post a Comment