Na. Kadala Komba Dodoma
Naibu
Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe.
Patrobas Katambi, amewataka vijana kujitabua ,kuwa na uthubutu pamoja
na kujiwekea malengo ,Amesema uwezi kupewa lifti kama umekaa nyumbani
wakatio unasafari ya kwenda Daresalam lazima usogee Barabarani ukisimama
tu wanajua wewe ni msafiri utapewa lifti .
Hayo
yamejili jijini Dodoma Wilaya ya Chamwino wakati wa Kongamano la Vijana
la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya
Vijana.
Katambi Amesema Lengo la Kongamano hili ni kumwezesha kijana kujitambua na atambue nafasi yake kwenye Jamii,
“kila kijana anatakiwa kupambana kivyake lakini akumbuke Serikali yetu ni Moja”
Aidha Naibu Waziri Katambi amewasisitiza Vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kuwa Tegemezi kwa Wazazi wao,
Ameongeza
kuwa Vijana wengi wanafikra ya utegemezi hawataki kufanya kazi hawataki
kujituma, Amesema Kama mnavyofahamu, vijana duniani kote ndio
wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kujenga uchumi wa
mataifa yao.
"Ili tuwe
na Taifa lenye Nguvu tunahitaji Vijana wachapakazi wanao jituma hata
vitabu vya Dini vimewataka Vijana kufanya kazi” Alisema Mhe. Katambi
Kwa
upande wake Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora. Amewasisitiza
Vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali
Amesema Serikali hii ya hawamu ya sita imejipanga kutokomeza dibwi la
Vijana wasio na kazi za kufanya, wasio na Ajira.
"Ajira
inaweza ikawa kwenye kilimo inaweza kuwa kwenye mifugo au kwenye Boda
Boda na mama lishe, ndiyo maana tumekutana hapa kwa lengo la kujengana
kupitia haya mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya
Maendeleo ya Vijana.
Aidha
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amewapongeza Vijana kwa kuwa na
mwitikio Mkubwa wamejitokeza zaidi ya Vijana mia Tatu ambao watapatiwa
mafunzo mbalimbali namna ya kupambana na fursa tunataka Vijana wajiajili
wenyewe.
Naibu
Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe.
Patrobas Katambi
Akizungumza na vijana katika kongamano la Vijana wilaya ya Chamwino
Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora Akitoa pongenzi kwa vijana waliyojitokeza kuuzulia kongamano la vijana jimboni kwake
Madiwani waliyouzulia kongamano la vijana
0 Comments:
Post a Comment