Na Moreen Rojas Dodoma
Hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni.
Kwa
upande wa usambazaji Serikali ina makubaliano ya kimataifa Televisheni
Mtando ya Nuella (Nuella Online TV) ya nchini Uholanzi kununua na
kuonesha Filamu za Kitanzania, na hadi sasa kuna filamu tisa (9)
zinaonyeshwa huko.
Hayo
yamesemwa na Dkt.Kiagho Kilonzo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika
kuelekeza utekelezaji wa mwaka wa fedha 2022/2023.
Aidha
ameongeza kuwa Dira ya Bodi ya Filamu ni: Kuwa na Tasnia ya Filamu
Shindani kwa Maendeleo ya Taifa na kupunguza umasikini (Vibrant and
competitive Film industry for national development and poverty
alleviation).
Dhima ya
Bodi ya Filamu ni: Kuweka mazingira bora na wezeshi kwa ukuaji wa Tasnia
ya Filamu. (To create conducive and enabling environment for film
industry prosperity).
Malengo ya bodi ya filamu ni kukuza Tasnia ya Filamu kwa:
- kuweka miongozo ya uundwaji wa Sera na Sheria za kuisimamia Sekta ya Filamu nchini,
- Kuongeza uzalishaji wa filamu za kitanzania na za kimataifa nchini Tanzania
- Kuimarisha uwekezaji katika Sekta ya Filamu
Kuendeleza uhifadhi wa kazi za filamu nchini.
Majukumu ya bodi ya filamu.
Kuishauri
Serikali masuala yote yanayohusu Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na
kuratibu Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza;
Kusimamia
na kuratibu utayarishaji/uandaaji, uhakiki wa Filamu na Michezo ya
Kuigiza pamoja na kuzipangia madaraja na kuzipa vibali; na
Kuandaa,
kuratibu na kuendesha warsha, vikao, mijadala na mafunzo ya kujenga
weledi kwa wadau wa filamu, utoaji wa tuzo na uendeshaji wa matamasha
mbalimbali.
Fursa za Ajira
Kwa
kipindi cha Januari hadi Disemba, 2021 pekee inakadiriwa kuwa
ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu (waigizaji,
waandaaji na watoa huduma). Kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja
(wastani wa watu 20, tamthilya moja wastani wa watu 100).
Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020.
Mfumo wa Kutoa Huduma za Bodi KIDIJITALI.
Taasisi
imeanzisha mfumo ambao unatoa huduma karibia zote za Bodi kwa wadau
wake (bila kulazimika kufika katika ofisi za Bodi) ikiwemo:
- vibali mbalimbali (uandaaji wa filamu, uhakiki, vitambulisho, nk)
- kuhifadhi taarifa za wadau,
- kuwatambua kupitia vitambulisho vinavyotolewa na Bodi.
Filamu za Kimkakati
Program
hii ina lengo la kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza
utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia (maeneo
mahsusi) ya nchi kwa lengo la kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa
kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali
waliyonayo. Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa
kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa
kama vile Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa
nchi mbalimbali barani Afrika.
Dkt.Kiagho
wakati akujibu maswali ya waandishi wa habari amesema kuwa kama bodi
wamejipanga kuhakikisha wanatoa maudhui mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja
na kuwapa semina wasanii chipukizi namna gani ya kujiuza kimataifa ili
kuweza kukua kibiashara kuendana na kasi ya ulimwengu ikiwa ni pamoja na
kulinda tamaduni zetu kama taifa kwa kuwa na vijana wanaojielewa.
Kwa
upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameipongeza bodi ya
filamu Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo imepelekea Tanzania
kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu Afrika na kuwaomba wawekezaji
wa ndani na nje kuungana na sekta hiyo ili kuweza kufika mbali zaidi
kwani tayari filamu zetu zimeshashinda tuzo mbalimbali nje ya nchi hii
ni kuonyesha ni kwa namna gani sekta ya filamu nchini inazidi kwenda
kimataifa.
|
0 Comments:
Post a Comment