Na Moreen Rojas Dodoma
Jumla
ya tani 8,959.023 za korosho ghafi zilibanguliwa ndani ya nchi kati ya
tani 240,158.753 zilizozalishwa sawa na 3.7% na jumla ya leseni 55 za
ununuzi wa korosho kwa ajili ya kusafishia nje ya nchi zilizotolewa
ikiwa ni ongezeko la kampuni 5 ukilinganisha na leseni katika msimu wa
2020/2021.
Hayo yamesemwa
na Fransis Afred Mkurugenzi wa bodi ya Korosho wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma lengo
ni kutoa taarifa ya itekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo kwa
mwaka 2021/2022 na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022/2023.
Aidha
ameongeza kuwa kiasi cha kilo 91,764 za mbegu bora za korosho zenye
thamani ya shilingi 275,292,000 zimesambazwa katika halmashauri 87
zinazolima korosho hapa nchini ikiwa ni mkakati mojawapo wa kufikia
uzalishaji wa korosho ghafi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/2026.
Wakulima
281,200 walisajiliwa kati ya wakulima 318,407 waliotarajiwa kusajiliwa
sawa na 88% jumla ya wakulima na wapuliziaji 1,304, Viongozi wa Amcos
703 pamoja na maafisa ugani 1,923 wamepatiwa mafunzo bora ya kilimo cha
korosho kwa kushirikiana na Tari _Naliendele "Amesema Afred.
Pikipiki
95 zenye thamani ya shilingi 297,514,236 zilizotolewa kwa maafisa ugani
ikiwa ni nyezo muhimu katika kuwafikia na kuwahudumia wakulima kwa
wakati.
Pamoja na hayo
jumla ya maafisa ugani 536 kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi,Ruvuma,Pwani na
Tanga waliweza kunufaika na mpango wa motisha ya shilingi 100,000 kwa
mwezi juu ya utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima takribani shilingi
milioni 200 zilitengwa kwa ajili hiyo.
Kiasi
cha tani 30,000 kinatarajiwa kubanguliwa hapa nchini kati ya tani
400,000 zinazotarajiwa kuzalishwa,jumla ya leseni 60 zinatarajiwa
kutolewa kwa msimu huu ambapo hadi sasa jumla ya kampuni 25
zimewasilisha maombi ya leseni " Amesema Afred.
Bodi
ya Korosho Tanzania inaendelea na maandalizi ya usimamizi wa masoko na
mauzo ya korosho ghafi ili kuhakikisha msimu wa mwaka 2022/2023 unakuwa
na mafanikio kwa wadau wa Tasnia ya korosho nchini.
Bodi
tayari imeanza kusajili na kutoa leseni kwa wanunuzi wa korosho ghafi
kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na kubangua nchini ambapo hadi
kufukia tarehe 07 oktoba 2022,jumla ya kampuni 48 zimesajiliwa na kati
yake kampuni 18 tayari zimepata leseni na zilizosalia zipo katika hatua
mbalimbali za kukamilisha upatikanaji wa leseni "Amesema Afred.
Bodi
itaendelea kushirikina na wadau wote katika mnyororo wa zao la korosho
kuhakikisha mkulima anazalisha na kuuza korosho zake kwa tija kwa
maendeleo ya tasnia ya korosho nchini.
0 Comments:
Post a Comment