Subscribe Us

UZINZI NA UASHERATI NI VYANZO VYA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE MAISHA YA MTU



“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Waebrania 13:4

 Siku zote mtu hutumikia adhabu ya kifungo na yapo madhara makubwa yatokanayo na vifungo vya uzinzi na uasherati

 UZINZI ni kufanya tendo la ndoa nje ya agano la ndoa kwa mtu aliye katika ndoa

UASHERATI ni kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa

BAADHI YA VIFUNGO VITOKANAVYO NA UZINZI NA UASHERATI

(1) - Kuungwa na kuwa mwili mmoja na kahaba 

“Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”.

1 Wakorintho 6:16

Unapofanya uzinzi au uasherati si tu unafanya dhambi bali pia roho zilizo ndani ya mtu uliyefanya naye uzinzi au uasherati zinaingia ndani mwako pia 
“Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu”.

1 Wakorintho 7:14

✓ Kama ana mapepo hayo mapepo yanaingia ndani yako

✓ Akiwa na roho ya kukataliwa na wewe unaanza kukataliwa

✓ Akiwa na roho ya kutokufanikiwa na wewe unaanza kutokufanikiwa

✓ Kila roho atakayokuwa nayo na wewe unakuwa nayo

✓ Ukizini na jini unakuwa mwili mmoja na jini

(2) - Unapoteza kibali na unakuwa mtu wa kukataliwa, kuzarauliwa unakuwa kitu kichafu 

“Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka”.

Maombolezo 1:18

(3) - Unaiua nafsi yako na kupelekea kukosa akili 

“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”.

Mithali 6:32

(4) - Nafsi inakamatwa na kufungwa 
“Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”

Mithali 6:26

(5) - Unaharibu nguvu ya agano la ndoa na kupelekea kutokua na ndoa imara, very kutokuolewa, kuvunjika kwa ndoa na kuachana.
6 Unafungua mlango wa mauti kwenye maisha yako kwenye kazi zako roho ya mauti inaanza kukuandama
Unafungulia mlango wa magonjwa ndani yako.
Uasherati haiombewi inahitaji uikimbie mpendwa subiri hadi uingie kwenye ndoa na yule wa kwako uliyekusudiwa na Mungu.




 

0 Comments:

Post a Comment