Na Peter Mkwavila CHAMWINO.
ASKOFU wa kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Kanda ya Kati Brayson Msanjila,amewashauri familia zinazogundulika kuwa na wagonjwa wa afya ya akili waache tabia ya kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji na wapiga ramli.badala yeke wawapeleke kwenye vituo vya afya ili wakapime afya zao kitaalamu zaidi.
Msanjila amesema hayo alipokuwa apokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chalinze nyama wilaya ya Chamwino kwenye ibada iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza mchungaji Saimon Sandiya aliyetimiza miaka 40 toka awe kwenye utumishi wake,
Ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Usharika wa Yerusalemu Chalinze Nyama Chamwino.
Askofu ameziomba familia hizo pindi zinapotokea kuwepo kwa mgonjwa wa afya ya akili,ni vizuri akapelekwa hosptalini badala ya huko kwa waganga na kwa wapiga ramli.
Alisema kuwa tatizo la afya ya akili likipatiwa matibabu haraka kwa asilimia kubwa linatibika haraka tofauti kama mgonjwa huyo akipelekwa kwa waganga wa kienyeji.
“Hivyo niziombe familia hususah huku vijijini pindi mnapogundua kuna tatizo hilo miongoni mwenu acheni kumkimbiza mgonjwa huyo kwa mganga wa kienyeji na wapiga ramli,bali wapelekeni hospitalini wakapatiwe matibabu ya kitaalam zaidi.
Alisema serikali kupitia hospitali zake kuna wataalamu wa kutosha kwa ajili ya magonjwa ya afya ya akili,hivyo hakuna sababu ya kuwapeleka watu wanaongudulika kuwa na tatizo hilo.
Awali akizungumza na wakazi hao wa kijiji hicho pia amewashauri wakulima kuhakikisha wanaandaa mashamba yao mapema ikiwemo na kuweka mbolea kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mbegu kwa wakati.
Naye Mchungaji Saiman Sandiya ambaye kiongozi wa kanisa hilo la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Usharika wa Yerusalemu Chalinze Nyama Chamwino.
Kwa upande wake amewataka wazazi na walezi ambao wana wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi kuwaendeleza kielimu zaidi badala ya kuwaweka majumbani.
Sandiya ambaye ametimiza miaka 40 ya uchungaji kwa kumtumikia Mungu,alisema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuwaendeleza kielimu ikiwemo na kwenye vyuo vya ufundi na kwa kufanya hivyo watakuwa wamewawekezea taaluma.
Alisema kuwa watoto hao wakianchwa bila kuendelezwa taifa litakuwa na tabaka la vijana wanaoweza kujikuta wakijiingiza kwenye makundi maovu kama vile panya road na mengineyo.
Mwisho.
0 Comments:
Post a Comment